“KWARESIMA YA
UKARIMU”
Tafakari ya
Kwaresima, Jumanne, Machi 21,
2017,
Juma la 3 la
Kwaresima
Dan 3:25,34-43;
Zab 25:4-9;
Mt 18:21-35
MSAMAHA
Injili ya leo
inatupa mfano wa jinsi ya kupokea na kutoa msamaha. Kinachovutia, ni rahisi
kusamehe zaidi ya kuomba msamaha. Kwakweli katika kuomba msamaha inahitaji kuwa
mwaminifu kwanza kwa kukubali kwamba nimekosa, ambapo mara nyingi ni jambo
ngumu kulifanya. Ni vigumu kuchukua jukumu kwa lile tulilokosa. Katika mfano
huu, huyu mtu anayeomba apewe muda ili aweze kulipa anaonekana kuwa mwaminifu.
“Anapiga magoti” mbele ya Bwana wake kwa huruma na kuomba apewe muda. Na huyu
Bwana wake anaonesha msamaha kwa kumsamehe deni lote ambalo lilikuwa kubwa
kuliko jinsi alivyo omba.
Lakini inaonekana
alikuwa muigizaji mzuri sana kwasababu mara tu ya kusamehewa deni hili kubwa,
anamkimbilia mtu ambaye alikuwa anamdai tena kiasi kidogo tu, na badala ya
kumuonesha huruma “anamrukia na kuanza kumpiga, akimdai, nilipe mali yangu”.
Msamaha kama ni wa kweli, unapaswa uingie kila mahali katika kila kitu
tufanyacho.
Je, waweza kuona
kosa lako na kusema samahani kwa mwingine?
Wakati unapo
samehewa, jambo hili linatoa fundisho ghani?
Je, waweza kutoa
msamaha na huruma kama wewe ulivyo samehewa?
Kama huwezi kjibu
“ndio” kwa maswali hayo, basi ujue mfano huu uliandikwa kwa ajili yako. Haya ni
maswali magumu kukutana nayo lakini ni maswali muhimu kama tunataka kutua
mizigo na kuwa huru. Tutafakari maswali hayo hapo juu na katika sala tutafiti
matendo yetu. Mimi na wewe tuna deni kubwa ambalo hatuwezi kulilipa (dhambi
zetu). Bwana wetu anatuita leo katika mahakama yake (Ekaristi). Kwa msaada wa
Roho Mtakatifu, tujenge tena upya uhusiano wetu na kuwa vyombo vya Amani.
Sala: Bwana,
ninakiri dhambi zangu. Lakini ninakiri kwa msaada wa mwanga wa neema na huruma
yako. Ninapo ipokea huruma hii katika maisha yangu, ninaomba unifanye mwenye
huruma kwa wengine. Nisaidie niweze kutoa msamaha kwa uhuru kamili bila kubaki
na kitu. Yesu nakumini wewe. Amina.
Tabia takatifu ya
Kwaresima: HURUMA-Bwana nisaidie niweze kuwa na haki na huruma kwa wote kama
wewe ulivyo kwa ajili yangu. Amina.
0 blogger-facebook:
Post a Comment