“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Alhamisi, Machi 23, 2017.
Juma la 3 la Kwaresima
Yer 7:23-28;
Zab 95:1-2, 6-9;
Lk 11:14-23
JE, TUME NYAMAZISHWA KUHUBIRI INJILI?
Leo, katika Injili Yesu analaumiwa kwa
kutoa pepo kwa kutumia mkuu wa pepo. Wapinzani wa Yesu walishindwa kuona kidole
cha Mungu ndani ya Yesu kwa huruma yake kwa wagonjwa. Hali hii inaonesha wazi
kutokuamini kwa Mafarisayo na viongozi wa Wayahudi kwamba Yesu ni Masiha.
Injili ya leo inaongeleo mtu ambaye alikuwa bubu kwasababu ya pepo. Wakati pepo
alivyotolewa na Yesu, huyu mtu aliyekuwa bubu alianza kuongea, watu wakashangaa
sana. Ni hakika kwamba huyu pepo alikuwa amemshika huyu mtu kiasi kwamba
alikandamizwa kabisa mpaka akashindwa kuongea. Baada ya kuwekwa huru kutoka
katika huyu pepo, ana anza kuongea kwa uhuru.
Ingawaje hatuwezi kuhisi uwepo wa pepo
katika hali kama hii, lakini katika hali fulani tunakutana na ukandamizaji kama
wa huyu pepo wa kutufanya tubaki kimya. Yule muovu anajaribu kutuogopesha kiasi
kwamba tunakuwa waoga kutangaza Injili kwa uhuru na kwa uaminifu, na kwa jinsi
Mungu anavyopenda ujumbe wake uwafikie watu. “pepo wa ububu” anaweza
kututawala, kutuchanganya au kutujaza hofu fulani wakati muda umefika wa
kushirikisha Imani yetu na wengine. Ingawaje ni vigumu kuanguka moja kwa moja
mikononi mwao, lakini mara nyingi tunajaribiwa kila mara na wao. Yesu ana nguvu
kamilifu juu ya pepo wa aina zote, yeye hasiti kuwanyamazisha pepo hao kama
ukimruhusu. Yesu anataka kutuweka huru ili tuweze kuongea kwa kuhubiri neno
lake la upendo bila kujibakiza ili wengine waweze kumfahamu yeye na upendo wake
mkamilifu. Mwache yeye akutumie kama moja ya chombo cha ukweli na upendo.
Sala: Bwana, wakati mwingine naingiwa na hofu na kuwa kimya na
kushindwa kutangaza neno lako vizuri kwa wale wahitaji. Wakati mwingine nahisi
kama nimefungwa kinywa kuongea, au kuchanganyikiwa niseme nini. Bwana naomba
unifungue kinywa changu niweze kuongea, Bwana wangu, ili niweze kuwa chombo
chako kitakatifu cha neno lako na kwa ujasiri na uaminifu niweze kutangaza neno
lako kwa wote walio wahitaji. Yesu, nakuamini wewe. Amina
0 blogger-facebook:
Post a Comment