Na. James Waibina.
Karibu Mpenzi Msomaji na mfuatiliaji wa Makala zetu katika Blog hii ya Fumbuka..
Leo katika Makala hii ya "Fursa kwa wote" ninakuletea njia zitakazo kusaidia ili uweze kuwa mbunifu katika biashara yako, tambua kuwa biashara ili ikue inahitaji ubunifu utakaokusaidia kubuni mbinu mbalimbali na kuhakikisha biashara yako inakuwa na mafanikio makubwa.
Yafuatayo ni mambo ya kufanya ili uweze kuwa mbunifu, karibu tuwe sote...
Yafuatayo ni mambo ya kufanya ili uweze kuwa mbunifu, karibu tuwe sote...
1. Jenga Urafiki na Watu
Kuwa na urafiki na watu ambao
wamefanikiwa kwenye biashara kama yako ni njia mojawapo ya kukusaidia kuwa
mbunifu.
Ukiwa na ukaribu na watu ambao
wanafanya biashara kama yako na wamefanikiwa utajifunza mambo mengi sana kutoka
kwao, pale ambapo wewe ulikuwa unakosea utajifunza na pale ambapo ulikuwa sio
bora utaumiza kichwa kubuni kitu kipya ambacho kitakufanya kuwa bora zaidi.
2. Jisomee Vitabu na Majarida.
Tafuta vitabu vya watu waliofanikiwa kwenye
biashara ambayo wewe unataka kuifanya, vitabu vimeeleza siri mbalimbali
zitakazokufanya kuwa mbunifu kwenye biashara yako, jitahidi sana kuwa msomaji
wa vitabu mbalimbali vinavyofundisha biashara kama unayofanya vitakujengea
uwezo mkubwa sana wa kuwa mbunifu kwenye biashara yako.
Vitabu vitakupa mbinu mbalimbali za kufanikiwa
kwenye biashara yako, kumbuka vitabu havipatikani bure lazima ununue kwahiyo hakikisha
unanunua vitabu na unavisoma ili uweze kuongeza maarifa zaidi.
3. Hudhuria Semina na Makongamano.
Watu wengi hawapendi kuhudhuria semina na
makongamano ya ujasiriamali lakini ngoja nikwambie kitu kama unataka kufanikiwa
kwenye maisha yako hakikisha unatafuta semina nyingi sana hata kwa kulipia
nenda kalipie ukajifunze utapata mawazo mengi sana ambayo yatakusaidia kuwa
mbunifu kwenye biashara yako, kwasababu utakuwa kila siku unapata mawazo mapya
utajikuta kila siku unajua njia za kuboresha biashara zako na hapo ndipo
ubunifu huzaliwa, lakini kama unafikiria ukianzisha tu biashara ndio basi,
utafeli sana kwenye biashara zako.
4. Kuwa na Mentor
Mentor ni Mlezi Mshauri, hakikisha una mlezi kwenye
biashara yako, kama hauna mlezi ni kazi sana kufanikiwa kwenye biashara tafuta
mentor ambae atakuwa anakuongoza kwenye biashara yako, huyo anakuwa anakupa
mawazo mapya na ushauri wa kufanikiwa kwenye biashara yako,utafanikiwa sana na
utakuwa mbunifu.
Hizo ndio njia pekee unazoweza kuzitumia kuwa
mbunifu.
Ahsante.
Ahsante.
Kwa Maoni /Ushauri: Tuwasiliane kupitia
0713515059 -(WhatsApp) au jameswaibina@fumbuka.co.tz
0 blogger-facebook:
Post a Comment