Na.
James Waibina.
Habari ndugu msomaji wa
makala zangu katika blog hii ya Fumbuka, karibu tena siku ya leo tuweze
kujifunza zaidi kuhusu Ndoa na Mahusiano, leo tutazungumzia mahusiano.
Mahusiano ni sehemu kubwa
sana katika kufanikiwa au kutokufanikiwa kwenye maisha yako, kama hauko kwenye
mahusiano mazuri unaweza kukuta ndoto zako zinakufa na unashindwa kuwa yule mtu
ambae umepanga kuwa kwenye maisha yako, lakini pia kama ukiweza kuyatumia
mahusiano vizuri pia yanaweza kuwa sehemu ya kufanikiwa kwenye maisha yako.
Watu wengi sana hasa vijana
wako kwenye mahusiano yasiokuwa na tija lakini wanashindwa kujinasua huko kwa
kuogopa kuumia au kumuumiza mwenzake na ni kweli unajua muda fulani kwenye
maisha unaweza kuwa na mtu ambae umemzoea kabisa anakufanyia mambo ambayo
yanakurudisha nyuma lakini unashindwa kumuacha kwasababu unaogopa maumivu, leo katika
makala hii nitakufundisha jinsi ya kumuacha mpenzi wako ambae hana tija kwenye
maisha yako bila kumsababishia maumivu.
Yawezekana upo katika Mahusiano yasiyo na tija kwako na unashindwa kuvunja mahusiano hayo, Tumia njia zifuatazo kuvunja uhusiano huo:-
1. Punguza
Mawasiliano Nae
Njia ya kwanza kabisa ya
kuacha mahusiano yasio na tija bila kusababisha maumivu ni kupunguza mawasiliano,
kama mlikuwa mnawasiliana mara tano kwa siku anza kufanya mara tatu kwa siku, baada
ya muda fanya mara mbili, baadae tena mara moja, najua utapokea maswali mengi
mara ooh mbona siku hizi hunipigiii jibu rahisi tu niko busy au sina vocha, mwisho
wa siku atazoea.
2. Punguza
Muda Wa Kukutana Nae
Kama mlikuwa mnaonana mara
mbili kwa wiki anza kumpa nafasi ya kuonana mara moja kwa wiki, halafu ongeza
kazi za kufanya ili hata akisema akutafute yeye atakukuta tu uko kwenye kazi
nyingine najua utapokea maswali mengi sana, cha msingi ongea naye vizuri mwambie
kuna majukumu yameongezeka mwanzo itakuwa ngumu lakini mwisho wa siku atazoea
tu. wewe umeshaona kuwa hayo mahusiano hayakufikishi kwenye ndoto zako.
3. Fanya
Mazoezi Sana
Kama ulikuwa huna tabia ya
kufanya mazoezi ya viungo anza kufanya mazoezi ya viungo, mazoezi yanakufanya
uwe busy muda mwingi na yanakuondolea mawazo yote, hii itakufanya uwe mtulivu
sana siku zote.
4. Punguza
Matumizi Kwake na Anza Kuweka Akiba
Hapa inabidi uwe mtu wa
sina hela,punguza kabisa matumizi kwake halafu anza kuweka akiba,kama ulikuwa
unamfanyia manunuzi mara kwa mara punguza halafu weka akiba,ili ikusaidie
baadae.
5. Mfanye
Awe Rafiki Yako
Ukitaka kuachana na
mahusiano yasio na tija haina haja ya kumfanyia visa mwenzako, au kumuonyeshea
kuwa humtaki tena hapana inaweza kukuumiza wewe zaidi au ikamuumiza yeye zaidi,
maisha siku zote hayaeleweki, unaweza kuona leo mtu hana msaada kwako lakini
siku nyingine akawa msaada kwako, sasa msiachane vibaya hata kama umegundua
kuwa mahusiano hayo hayakufikishi kwenye ndoto zako, cha msingi wewe mfanye awe
rafiki yako, tena ikiwezekana kama ulikuwa unamuita majina ya kimapenzi muda
wote anza kumuita rafiki. itakuwa ngumu mwanzo lakini atazoea tu.
6. Anza
Kumshauri Sana Kuhusu Maisha Kuliko Mapenzi
Tumia muda wako mwingi kila
mnapokutana kuzungumzia maisha na ndoto zenu, mshauri sana kuhusu maisha kuliko
mapenzi utaona kuna nguvu fulani hivi ambayo ilikuwa imezoeleka itaanza
kupungua siku hadi siku na mwisho wa siku mnaachana kirafiki kabisa na kila mtu
anaendelea na maisha yake huku mkiwa mnaongea kama kawaida.
Kwenye maisha usikubali
kabisa mahusiano yavuruge ndoto zako na malengo yako ya kimaisha, ukiona tu uko
kwenye mahusiano ambayo unaona yanapokupelekea ni kupoteza ndoto zako anza
kuyaacha mapema sana.
Ahsante.
Kwa Maoni /Ushauri: Tuwasiliane kupitia
0713515059 -(WhatsApp) au jameswaibina@fumbuka.co.tz
0 blogger-facebook:
Post a Comment