SOMO 1
Isa. 7:10 – 14
Bwana
alisema na Ahazi akinena, Jitakie ishara ya Bwana, Mungu wako; itake katika
mahali palipo chini sana, au katika mahali palipo juu sana. Lakini Ahazi
akasema, Sitaitaka, wala sitamjaribu Bwana. Naye akasema, Sikilizeni sana, enyi
nyumba ya Daudi; Je! Ni neno dogo kwenu kuwachosha wanadamu, hata mkataka
kumchosha Mungu wangu pia? Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama,
Bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake
Imanueli.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 40:6 – 10 (K) 7 , 8
(K)
Tazama, nimekuja, Ee Bwana, kuyafanya mapenzi yako.
Dhabihu
na matoleo hukupendezwa nazo,
Masikio
yangu umeyazibua,
Kafara
na sadaka za dhambi hukuzitaka.
Ndipo
niliposema, Tazama nimekuja. (K)
Katika
gombo la chuo nimeandikiwa
Kuyafanya
mapenzi yako,
Ee
Mungu wangu, ndiyo furaha yangu;
Naam,
sheria yako imo moyoni mwangu. (K)
Nimehubiri
habari za haki katika kusanyiko kubwa,
Sikuizuia
midomo yangu; Ee Bwana, unajua. (K)
Sikusitiri
haki yako moyoni mwangu;
Nimetangaza
uaminifu wako na wokovu wako.
Sikuficha
fadhili zako wala kweli yako
Katika
kusanyiko kubwa. (K)
SOMO 2
Ebr. 10:4 – 10
Haiwezekani
damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi. Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema,
Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari; Sadaka za
kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; Ndipo niliposema, Tazama
nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) niyafanye mapenzi yako, Mungu.
Hapo
juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi
hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati), ndipo
aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili
kusudi alisimamishe la pili. Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa
mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO
Yn. 1:14
Neno
alifanyika mwili, akakaa kwetu, nasi tukaona utukufu wake.
INJILI
Lk 1:26-38
Mwezi
wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina
lake Nazareti, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake
Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu. Akaingia
nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema. Bwana yu pamoja nawe. Naye
akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya
namna gani? Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa
Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita
Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye ju, na Bwana Mungu atampa kiti
cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na
ufalme wake utakuwa hauna mwisho. Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno
hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia
juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo
hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. Tena, tazama, jamaa
yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na
mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa; kwa kuwa hakuna neno
lisilowezekana kwa Mungu. Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na
iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
0 blogger-facebook:
Post a Comment