728x90 AdSpace

­
Latest News
March 8, 2017

TAFAKARI YA KWARESIMA: Ombeni Nanyi Mtapewa

“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Alhamisi, Machi 9, 2017.
Juma la 1 la Kwaresima

Est C:12, 14-16, 23-25;
Zab 138:1-3, 7-8
Mt: 7:7-12

OMBENI NANYI MTAPEWA!

Mara baada ya kuwafundisha Wanafunzi wake kusali, leo Yesu anawaambia: “ombeni nanyi mtapokea …” Baba yetu wa Mbinguni anatupatia kwa neema zake yale yote tunayo muomba hata kwa jinsi tusio tegemea, na kwa wote wanaojua na kutegemea upendo wake, husali kwa hakika. Sala inatokana na upendo wetu kwa Mungu na upendo wake kwetu sisi. Hili linatusaidia kushirikisha upendo wake kwa wengine, kwani Mungu amemimina upendo wake ndani ya Roho zetu kwa njia ya Roho Mtakatifu. (Warumi 5: 5). 

Yesu ana hakika kabisa kwamba tutakapo omba tutapokea, tutakapo tafuta, tutapata, na tutakapo bisha hodi, tutafunguliwa mlango. Mara nyingi tunaweza kuomba na kuomba, lakini tunaona sala zetu hazijibiwi, katika hali ya jinsi tulivyo ziomba. Hili linaleta swali “sasa nisalije na nisali kwa ajili ya nini?”. Lakini kila sala au ombi tunalosema linapaswa liwe kwa ajili ya mapenzi ya Mungu yafanyike, hakuna zaidi, wala hakuna chakupunguza. Ni kwa ajili tu ya mapenzi yake kamili yatimie.

Tutafakari leo, jinsi tunavyosali. Tubadili sala zetu ili ziwe zinatafuta mambo mazuri ambayo Mungu anataka kuyaweka kwetu. Itakuwa ngumu mara ya kwanza kuachana na mapenzi yetu na mawazo yetu, lakini mwishoni tutabarikiwa na mambo mengi mazuri kutoka kwa Mungu. 

Sala: Bwana, ninasali mapenzi yako yatimizwe katika kila kitu. Ninatamani kukabidhi kwako, na kuamini mpango wako mkamilifu. Nisaidie Bwana kuachana na mawazo yangu peke yangu na kutafuta ya kwako daima. Yesu, nakuamini wewe. Amina. 

Tabia ya Kwaresima: SUBIRA-Bwana nisaidie niweze kuwa na tabia ya subira, ninaomba niwe na subira kwa mapenzi yako yatimizwe katika maisha yangu bila kuwa na haraka ya kutaka yakamilike. Amina.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: TAFAKARI YA KWARESIMA: Ombeni Nanyi Mtapewa Rating: 5 Reviewed By: Unknown