UTANGULIZI
Ifuatayo ni mada fupi kuhusu namna ya kusali rozari
takatifu ya Bikira Maria, pamoja na sala kuu zinazosaliwa wakati wa sala hii ya
rozari. Wakati wa kusali unaweza kuongeza sala nyingine zifaazo kadri ya
nafasi. Rozari takatifu husaliwa na wakristu kutafakari maisha ya Yesu na Maria
yaani Fumbo la Ukombozi, hasa kipindi cha mwezi Mei na Oktoba. Inahimizwa
kuisali kama familia kila siku. Tusali rozari tupate amani, wakosefu waongoke
na wasiomjua Yesu Kristu wamjue na kuokoka.
Maelezo
Ya Jumla
Anza kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu
katika taswira (picha) yake Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba (gusisha msalaba
huo kwenye paji la so, kifuani, bega la kushoto na kwa kutumia msalaba wa
rozari takatifu huku ukiwa unasema “Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho
Mtakatifu, Amina”.
Taja kwa ufupi nia za Rozari hii. Tangaza nia hizo
kwa sauti kama mnasali wengi kwa pamoja, Mfano, “Tusali kuombea amani katika
nchi yetu na ulimwenguni kote" au tutolee rozari hii kuwaombea wagonjwa
wetu: au :tuwaombee wote walioomba tuwaombee" nk. Hiyo ni mifano tu. Au
unaweza kutoa mambi kuendana na tendo lililotangazwa kwenye kumi husika la
tendo la rozari, au namna nyingine itakayofaa.
Baada ya Sala ya Nasadiki pamoja na ya Baba Yetu,
tunamwomba Mungu (Utatu Mtakatifu) fadhila za Imani, Matumaini na Mapendo,
zikiambatana na Salamu Maria tatu. Mojawapo ya maneno yafuatayo hutumika:
“Mungu Baba utuongezee Imani. Salamu Maria, ……
Mungu Mwana utuongezee matumaini, Salamu Maria, …… Mungu Roho Mtakatifu washa
nyoyo zetu kwa mapendo yako, Salamu Maria, …..”
Au;
“Utuongezee Imani ee Bwana, Salamu Maria,….
Utuongezee matumaini ee Bwana, Salamu Maria,…. Uwashe nyoyo zetu kwa mapendo
yako ee Bwana, Salamu Maria, …..”
Au;
“Salamu e uliyechaguliwa na Mungu Baba, Salamu
Maria,….. Salamu e Mama wa Mungu Mwana, Salamu Maria,….. Salamu e Mchumba wa
Mungu Roho Mtakatifu, Salamu Maria,……”
Nk.
SALA ZA
ROZARI TAKATIFU
Kanuni Ya
Imani
Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, mwumba mbingu na
dunia. Na kwa Yesu Kristu, Mwanaye wa pekee, Bwana wetu; aliyetungwa kwa Roho
Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato,
akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu; siku ya tatu akafufuka katika
wafu; akapaa mbinguni; amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; toka huko atakuja
kuwahukumu wazima na wafu. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu
katoliki, ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, uzima
wa milele. Amina.
Baba
Yetu...
Baba Yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe;
ufalme wako ufike, utakalo lifanyike, duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate
wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi
waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina
Salamu
Maria...
Salamu Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe.
Umebarikiwa kuliko wanawake wote. Na Yesu Mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu.
Amina.
Atukuzwe
Baba...
“Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, kama
mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina”;
Ee Yesu
Wangu...
Ee Yesu wangu, utusamehe dhambi zetu, utuepushe na
moto wa milele, ongoza roho zote mbinguni, hasa za wale wanaohitaji huruma yako
zaidi”;
Tuwasifu
Milele...
“Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosef”.
Damu Ya Kristu..
Damu ya Kristu, iziopoe roho zinazoteseka toharani,
izitie nuru ya uzima wa milele. Amina.
Au;
Raha Ya
Milele..
Raha ya milele uwape ee Bwana, na mwanga wa milele
uwaangazie. Wapumzike kwa amani. Amina.
NB: Kama muda unatosha uimbwe wimbo
wa Bikira Maria japo ubeti mmoja kabla ya kutangaza tendo linalofuata (kila
baada ya makumi mamoja)
Litania
Ya Bikira Maria
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utuhurumie
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utusikie
Kristo utusikilize
Mungu Baba wa
Mbinguni, Utuhurumie
Mungu Mwana Mkombozi wa
dunia
Utuhurumie
Mungu Roho
Mtakatifu Utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu
Mmoja
Utuhurumie
Maria Mtakatifu utuombee
Mzazi Mtakatifu wa
Mungu
utuombee
Bikira Mtakatifu Mkuu wa
mabikira
utuombee
Mama wa
Kristo
utuombee
Mama wa neema ya
Mungu
utuombee
Mama Mtakatifu
sana
utuombee
Mama mwenye usafi wa moyo
utuombee
Mama mwenye
ubikira
utuombee
Mama usiye na
doa
utuombee
Mama
mpendelevu
utuombee
Mama
mstajabivu
utuombee
Mama wa
Muumba
utuombee
Mama wa
Mkombozi
utuombee
Mama wa
Kanisa
utuombee
Bikira mwenye
utaratibu
utuombee
Bikira mwenye
heshima
utuombee
Bikira mwenye
sifa
utuombee
Bikira mwenye
uwezo utuombee
Bikra mweye
huruma
utuombee
Bikra mwaminifu
utuombee
Kioo cha
haki
utuombee
Kikao cha
hekima
utuombee
Sababu ya furaha yetu utuombee
Chombo cha
neema
utuombee
Chombo cha
kuheshimiwa
utuombee
Chombo bora cha
ibada
utuombee
Waridi lenye
fumbo
utuombee
Mnara wa
Daudi
utuombee
Mnara wa
pembe
utuombee
Nyumba ya
dhahabu
utuombee
Sanduku la
Maagano
utuombee
Mlango wa
Mbingu
utuombee
Nyota ya
asubuhi
utuombee
Afya ya
wagonjwa
utuombee
Kimbilio la
wakosefu
utuombee
Mtuliza wenye huzuni
utuombee
Msaada wa
waKristo
utuombee
Malkia wa
Malaika
utuombee
Malkia wa
Mababu
utuombee
Malkia wa
Manabii
utuombee
Malkia wa
Mitume
utuombee
Malkia wa
Mashahidi
utuombee
Malkia wa Waungama
dini
utuombee
Malkia wa
Mabikira
utuombee
Malkia wa Watakatifu wote
utuombee
Malkia uliyepalizwa
Mbinguni
utuombee
Malkia wa Rozari
takatifu
utuombee
Malkia wa
amani utuombee
Mwanakodoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,
Utusamehe ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za
dunia,
Utusikilize ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,
Utuhurumie.
Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu,
Tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe
Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako afya
ya roho na mwili siku zote; na kwa maombezi matukufu ya Maria Mtakaatifu
Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya saa, tupate na furaha za milele. Kwa
Kristo Bwana wetu, Amina.
Salamu
Malkia...
Salamu Malkia, Mama mwenye huruma, uzima, tulizo na
matumaini yetu, salamu. Tunakusihi hapa ugenini sisi wana wa Eva. Tunakulilia
tukilalamika na kuhuzunika bondeni huku kwenye machozi. Haya basi, Mwombezi
wetu, utuangalie kwa macho yako yenye huruma. Na mwisho wa ugeni huu,
utuonyeshe Yesu, mzao mbarikiwa wa tumbo lako. Ee mpole, ee mwema, ee
mpendelevu, Bikira Maria.
Kumbuka...
Kumbuka, ee Bikira Maria mwenye rehema, tokea
zamani zote haitambulikani kumeachwa mwenye aliyekimbilia ulinzi wako, mwenye
aliyetaka msaada wako, mwenye aliyetaka maombezi yako. Nami nimetumaini kwako,
nimekimbilia kwako, ee Mama yangu, Bikira asiye na mfano, nimekuja kwako,
nasimama mbele yako mimi mwenye dhambi. Mama wa Neno wa Mungu, usiyachukie
maneno yangu, uyapokelee, uyasikilize, ukanifanyizie. Amina.
Sala Kwa
Mtakatifu Yosefu (mwezi
wa kumi isaliwe baada ya rozari)
Ee Mt. Yosefu mwenye heri, tunakimbilia kwako
katika masumbuko yetu, na kisha omba shime ya Mchumba wako Mtakatifu, tunaomba
pia kwa matumaini usimamizi wako. Kwa ajili ya mapendo uliyompenda Bikira
Mtakatifu Mzazi wa Mungu, na kwa ajili ya kumtunza Mtoto Yesu, twakuomba sana,
utuangalie kwa wema sie tuliokuwa fungu lake Yesu Kristu, tukakombolewa kwa
damu yake. Tusimamie katika masumbuko yetu kwa enzi na shime yako.
Ee Mlinzi amini wa jamaa takatifu, uwakinge watoto
wateule wa Yesu Kristu. Ee Baba uliyetupenda mno tuepushe na kilema chochote
cha madanganyo na upotevu. Ee kinga yetu mwezaji, utusimamie huko juu mbinguni
ulipo, tunaposhindana na wenye nguvu wakaao gizani. Kama vile siku za kale
ukamwopoa Mtoto Yesu katika hatari ya kuuawa, na leo hivi likinge Kanisa
Takatifu la Mungu katika mitego ya adui, na katika shida yote; mtunze daima
kila mmoja wetu, tufwate mfano wako, ili tupate na msaada wako, kukaa na
utakatifu maisha, kufa kifo chema, na kupata mbinguni makao ya raha milele.
Amina.
Tunaukimbilia...
Tunaukimbilia,
ulinzi wako, Mzazi Mtakatifu wa Mungu. Usitunyime tukikuomba katika shida zetu,
utuokoe siku zote kila tuingiapo hatarini, ee Bikira mtukufu na mwenye baraka.
Amina.
Amina 🙏
ReplyDeleteAmina
ReplyDeleteAmen
ReplyDeleteAmina
ReplyDelete