SOMO 1
Dan. 9:4 – 10
Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha,
ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake; tumefanya
dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha
maagizo yako na hukumu zako; wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii,
ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, na
watu wote wa nchi.
Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu
sisi kuna haya ya uso, kama hivi leo; kwa watu wa Yuda, na kwa wenyeji wa
Yerusalemu, na kwa Israeli wote, walio karibu na hao walio mbali, katika nchi
zote ulikowafukuza, kwa sababu ya makosa yao waliyokukosa. Ee Bwana, kwetu sisi
kuna haya ya uso, kwa wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, kwa sababu
tumekutenda dhambi. Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa
tumemwasi; wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu, kwa kwenda katika sheria
zake, alizoziweka mbele yetu kwa kinywa cha watumishi wake, manabii.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 79:8 – 9, 11, 13 (K) 103:10
(K) Usitutende sawasawa na hatia zetu,
Ee Bwana.
Usikumbuke juu yetu maovu ya baba zetu,
Rehema zako zije kutulaki hima,
Kwa maana tumedhilika sana. (K)
Ee Mungu wokovu wetu utusaidie.
Kwa ajili ya utukufu wa jina lako.
Utuokoe, utughofiri dhambi zetu,
Kwa ajili ya jina lako. (K)
Kuugua kwake aliyefungwa na kuingia
mbele zako.
Kwa kadiri ya uweza wa mkono wako.
Uwahifadhi wana wa mauti.
Na sisi tulio watu wako, na kondoo za
malisho yako,
Tutakushukuru milele;
Tutazisimulia sifa zako kizazi kwa
kizazi. (K)
SHANGILIO
Mt. 4:4
Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila
neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
INJILI
Lk. 6:36:38
Yesu aliwaambia wafuasi wake: Iweni na
huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma. Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa;
msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa. Wapeni watu kitu,
nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata
kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifruani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile
mpimacho ndicho mtakachopimiwa.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo. MASOMO YA MISA, MACHI 13, 2017
JUMATATU, JUMA LA 2 LA KWARESIMA

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
0 blogger-facebook:
Post a Comment