KUHUSU ELIMU YAKE
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amefunguka tuhuma zinazozushwa kupitia mitandao ya kijamii na watu mbalimbali kuhusu elimu yake na zinazoeleza kuwa amefoji cheti cha mtu mwingine.
Akizungumza kwenye kikao cha kamati ya ushauri wa Mkoa (RCC) RC Makonda ameeleza kuwa kinachogombaniwa siyo Makonda bali ni kiti alichokalia (UKUU WA MKOA), hivyo ameeleza kuwa nafasi yake ya ukuu wa Mkoa amepewa na Mungu.
Na kufafanua kuwa hatakama angepata sifuri au daraja la kwanza katika masomo yake, Mungu angetaka awe Mkuu wa Mkoa angekuwa tu, kwani Mungu ndiye anapanga kila kitu na kuongeza kuwa yupo imara kuliko alivyokuwa jana.
KUTISHWA KWA WAZAZI WAKE
Pia RC Makonda amefunguka kuhusu kutishwa kwa baba yake mzazi, pia kuna watu walikwenda eneo analoishi baba yake na mama yake mzazi na kupiga picha, ili wakaoneshe nyumba anayoishi mzazi wake.
KUHUSU KUITWA SHOGA NA MGUMBA
RC Makonda ameeleza kuwa watu wamekuwa wakimtolea lugha chafu kuhusu uzazi wake na kumuita mgumba kwa kuwa hana mtoto na wengine wamekuwa wakimuita shoga, amefunguka na kusema kuwa haoni tusi jipya.
RC Makonda amesema ipo siku watu wataulizwa kuhusu matendo wanayoyafanya duniani kilasiku, hawana budi kuwa makini na matendo yao.
KUHUSU DAWA ZA KULEVYA
RC Makonda ameeleza kuwa tangu aianze vita ya dawa za kulevya yameibuka mengi na kusisitiza kuwa hatoacha ataendelea kwani wapo wanaoshukuru kuanza kwa vita hiyo na kuhoji kwanini haikuanza mapema kwani imeokoa maisha ya wengi, kuhusu maendeleo ya vita hiyo RC Makonda amesema kuwa mashamba ya bangi yanateketezwa kila uchwao, siku mbili zilizopita wamekamatwa watu 100 na kete 400 za dawa hizo pia zimekamatwa.
0 blogger-facebook:
Post a Comment