Tatizo hili huwakumba watu
wengi sana kwenye jamii yetu lakini kwa bahati mbaya watu wengi huchukulia ni
jambo la kawaida kitu ambacho baadae hupelekea watu wengi kuingia kwenye
matatizo makubwa ya kiafya hasa kwenye mfumo wa uzazi na mfumo wa chakula.
Maumivu
Chini Ya Kitovu Hutokea Kama Ifuatavyo:-
Yapo yale ya chini ya
kitovu katikati, kushoto na kulia. Kwa wanawake maumivu ya kushoto na kulia
yapo ya aina mbili. Kuna yale ambayo yanakuwa upande mmoja lakini husambaa kwa
urefu wa sentimita mpaka nne na inaweza ikawa upande mmoja au pande zote mbili
lakini yapo mengine chini ya kitovu ambayo yanaweza yakawa upande mmoja au
pande zote mbili bila kusambaa kwa marefu.
Kuna maumivu mengine chini
ya kitovu huwapata wanawake wakati tu wanaposhiriki tendo la ndoa kwa ndani ya
uke au chini ya kitovu. Pia yapo ambayo huwapata wanawake wakati wameinama,
wakati wa kunyanyua vitu vizito, wakati wa kucheka au kuimba na wakati mwingine
wakiwa wamelala kifudifudi.
Maumivu
chini ya Kitovu Yanaashiria Matatizo Gani Kwa Wanawake?
1. Mirija ya uzazi kujaa
maji mazito na machafu ambayo huzuia yai kutembea kwenye mirija ya uzazi.
Mwanamke ambaye amewahi kuambiwa na daktari kwamba anatakiwa asafishwe kizazi
chake/mirija ya uzazi na wakati huo huo anasikia maumivu chini ya kitovu
kushoto na kulia au upande mmoja kuna uwezekano akawa na tatizo la mirija ya
uzazi kuziba kutokana na kujaa maji machafu.
2. Kutokukomaa kwa mayai ya
uzazi. Hii husababisha vifuko vya mayai ya uzazi kuvimba(ovaritis) na kumletea
mwanamke maumivu chini ya kitovu mithili ya kichomi. Mwanamke ambaye anamaumivu
chini ya kitovu na wakati huo huo ana matatizo ya hedhi mfano hedhi kukoma au
kutokuwa na mpangilio maalum kunauwezekano mkubwa akawa na tatizo la vifuko
vyake vya mayai ya uzazi kutokomaza mayai na hivyo mayai kutotoka kwenye vifuko
hivyo na kusababisha kuvimba na hatimaye kumsababishia mwanamke maumivu makali
mithili ya kichomi.
3. Kuvimba kwa kuta za mji
wa mimba na kuta za mirija ya uzazi (PID/Pelvic Inflamatory Disease). Mwanamke
anayesikia maumivu chini ya kitovu katikati na pembeni kwa wakati mmoja na
wakati huo huo akawa anatokwa na uchafu mzito mithili ya maziwa mtindi
kunauwezekano akawa na PID hasa hasa kama amewahi kukumbwa na tatizo la
kuharibika kwa mimba kabla haijafikisha miezi mitano.
4. Afya mbovu ya kibofu cha
mkojo ikiambatana na matatizo ya maambukizi kwenye mfumo mzima wa mkojo (UTI).
Maumivu chini ya kitovu yanayohusisha afya mbovu ya kibofu cha mkojo huambatana
na mgonjwa kutoa haja ndogo kidogo sana ila mara kwa mara.
Maumivu
chini ya kitovu kwa wanaume huashiria nini?
Maumivu chini ya kitovu kwa
wanaume huashiria pia tatizo la tezi dume liitwalo Prostatitis yaani kuvimba
kwa tezi dume. Maumivu haya hujikita kwenye shina la uume na huashiria tatizo
hili hasa kama mwanaume anakwenda haja ndogo mara kwa mara nyakati za usiku na
umri ukiwa unaelekea miaka 50 au zaidi.
Dalili nyingine ambatano ni
kutoa haja ndogo ambayo ina kasi ndogo sana tofauti na kawaida, ikiambatana na
maumivu ya kiuno na mgongo, kuvimba kwa korodani, haja ndogo inayoambatana na
usaha na damu, maumivu ya uume wakati wa kufika kileleni, na damu katika maji
ya uzazi (semen)
Kwa wanaume, maumivu haya
ya chini ya kitovu huashiria pia tatizo ambalo kitaalamu hujulikana kwa jina la
Hernia ambapo waswahili tunaita ngiri.
Mwanaume anaposikia maumivu haya ya
chini ya kitovu ikiambatana na maumivu ya korodani, korodani moja kupungua na
nyingine kukua zaidi au zote mbili kukua au kupotea, ni dalili ya ugonjwa huu
ambao huharibu ubora wa uzalishwaji wa mbegu za kiume ambazo zaweza kuzalishwa
chache au ambazo hazina kasi ya kutosha kusafiri kwenye via vya uzazi vywa
mwanamke na hivyo mwanaume kupoteza uwezo wake wa kutungisha mimba.
Maumivu chini ya kitovu kwa
wanaume kama ilivyo kwa wanawake huashiria tatizo la maambukizi katika mfumo wa
haja ndogo yaani (Urinary Track Infection/UTI) ambapo dalili zake ni kama zile
za mwanamke hapo juu.
Hitimisho.
Vipimo na tiba vyahitajika
mapema bila kuchelewa ili kuepuka madhara makubwa katika mfumo wa uzazi, mkojo
na hata wa chakula
USISAHAU KUSHARE NA WENGINE
ILI WAPATE DARASA HILI…
nauluna ivi Kam umeshawahi kuharibikiwa na mimba afu ukawa unsonu hedhi yako Kama kawaida lakin hukapata na maumivu chini ya kitovu baada ya hedhi
ReplyDeleteTatizo la kuumwa chini ya kitovu baada ya hedhi inaashiria Nini
ReplyDeleteMm nasumbuliwa na tumbo chini ya kitovu
ReplyDeleteMaumivu ya tumbo wakati wa usiku kuamkia asubuhi inasababishwa na Nini?
ReplyDeleteWakati huo huendeshi Wala kusikia maumivu wakati wa haja ndogo...
Mke wangu alianza kutokwa na uchafu mweupe na baadae akapata tiba na mimi nikashaueiwa kutumia dawa ambapo nilitumia power
ReplyDeleteSef inj 5 na baada ya hapo tuliendelea na tendo kwa condom miez miwili then tukaanza bila condom lakini mwenzangu amekuwa akihisi maumivu chini ya kitovu hali inayotutatiza kuwa shida ni nini.
Naomba ushauri
Tiba kwa mwanamke ni IPI?
ReplyDeleteTiba yake ni ip kwa wanawake wenye matatzo Kama hayo?
ReplyDeleteNina maumivu ya tumbo usawa wakitovu upande wa kushoto kuelekea chini na juu na huongezeka zaidi pale ninapotoka kufanya sexy hii ni dalili ya ugonjwa gani?
ReplyDeletekuumwa na tumbo maumiv makali n ukeni maumivu na kujiskia kutapika ni ishara ya nini
ReplyDelete