“KWARESIMA YA UKARIMU”
Jumamosi, Machi 11, 2017,
Juma la 1 la Kwaresima
Kumb 26: 16-19;
Zab 119: 1-2, 4-5, 7-8;
Mt 5: 43-48
KUTAMANI KUWA MKAMILIFU!
Liturujia ya leo inalenga katika Sheria
ya Mungu, ambayo Mungu ametupa kwa njia ya Musa ili kuifuata kwa moyo na nafsi
nzima. Katika Injili, tunaona Yesu, analeta upendo wenye athari kubwa, zaidi
kuliko wowote ule ambao waliutenda kabla. Kumpenda kila mtu, bila kuwa na fikra
au sababu yeyote ile, bila kujali kama wao wanatupenda sisi au la, bila
kufikiria wanatuwazia mabaya au mazuri?
Yesu wakati alipokuwa dunia hii,
alikabiliwa na upinzani sana, kutoka kwa mamlaka ya kidini, kutoka kwenye
mamlaka ya kisiasa, kutoka mji wake mwenyewe, kutoka kwa baadhi ya wanafunzi
wake mwenyewe. Hata hivyo, yeye amewapenda daima wote. Ujumbe wake wa huruma au
wa kubadilika mara zote ulijawa na upendo mkuu. Hata juu ya Msalaba,
aliwatazama kwa huruma watesi wake. Upendo kwa Mungu na kwa jirani huenda
pamoja, na hauwezi kutenganishwa. Mt. Yohane anaweka wazi kwamba, “Mtu akisema,
“Nampenda Mungu,” naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo (1Yoh 4:20).
Leo tunapewa changamoto na upendo huu
wa Yesu Kristo. Tumekuwa mara nyingi sana watu ambao tunabagua wengine, juu ya
rangi, dini, jinsia, kabila, juu ya tabaka, utaifa, juu ya hadhi ya jamii,
utamaduni, elimu, kiasi cha mali ulicho nacho nk, Je, tunaweza kuamua kumwiga
Yesu kuanzia sasa na kuendelea? Je, tunaweza kuwapenda wale wote ambao
wametuumiza katika maisha yetu? Wale wanaotutesa kwasababu ya utamaduni wetu,
dini yetu,au mawazo yetu? Yesu alishinda haya yote kwa upendo wake, Je, sisi
twaweza kufanya hivyo tushinde kwa njia ya upendo?
Sala: Bwana, ninataka kuwa mtakatifu.
Ninataka kuwa mtakatifu kama wewe ulivyo mtakatifu. Nisaidie niishi kila wakati
kwa ajili yako. Ninatoa muda wangu wote kwa ajili yako. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
Tabia Takatifu ya Kwaresima: KUFIKIRI
NA KUONGEA-Bwana nisaidie nijifunze KUFIKIRI kabla ya KUSEMA. Ninaomba niweze
kutafakari kila kitu ninacho sema, na hivyo, kuachana na maneno yeyote yanayo
waumiza wengine. Amina.
0 blogger-facebook:
Post a Comment