SOMO 1
Yer. 18-18-20
Waliposema, Njoni na tufanye mashauri juu ya
Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye
hekima, wala neno halitampotea nabii. Njoni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala
tusiyaangalie maneno yake yoyote.
Niangalie, Ee Bwana, ukasikilize sauti ya
wanaoshindana nami. Je! Mabaya yalipwe badala ya mema? Maana wameichimbia nafsi
yangu shimo. Kumbuka jinsi nilivyosimama mbele zako, ili nisema mema kwa ajili
yao, nikaigeuze ghadhabu yako isiwapate.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 31:4-5, 13-15 (K) 16
(K) Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako, Ee Bwana.
Utanitoa katika wavu walionitegea kwa siri,
Maana Wewe ndiwe ngome yangu.
Mikononi mwako naiweka roho yangu;
Umenikomboa, Ee Bwana, Mungu wa kweli. (K)
Maana nimesikia masingizio ya wengi;
Hofu ziko pande zote.
Waliposhauriana juu yangu,
Walifanya hila wauondoe uhai wangu. (K)
Lakini mimi nakutumaini Wewe, Bwana,
Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu.
Nyakati zangu zimo mikononi mwako;
Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia. (K)
SHANGILIO
Lk. 8:15
Heri wale walishikao neno la Mungu katika moyo wao
mwema na unyofu, na wazaao matunda katika uvumilivu.
INJILI
Mt. 20:17-28
Yesu alipokuwa akipanda kwenda Yerusalemu
aliwachukua wale wanafunzi kumi na wawili faraghani; na njiani akawaambia,
Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemu; na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa
wakuu wa makuhani na waandishi nao watamhukumu afe; kisha watampeleka kwa
Mataifa wapate kumdhihaki, na kumpiga mijeledi na kumsulibisha; na siku ya tatu
atafufuka.
Ndipo mama yao wana wa Zebedayo akamwendea pamoja
na wanawe, akamsujudia, na kumwomba neno. Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia,
agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja
mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako. Yesu akajibu akasema, Hamjui
mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia,
Twaweza. Akawaambia, Hakika mtakinywa kikombe change; lakini kuketi mkono wangu
wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa waliowekewa
tayari na Baba yangu.
Na wale kumi waliposikia, waliwakasirikia wale
ndugu wawili. Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa
huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini haitakuwa hivyo
kwenu; bali mtu yeyote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; na
mtu yeyote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; kama vile Mwana
wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumikia na kutoa nafsi yake iwe fidia ya
wengi.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
0 blogger-facebook:
Post a Comment