“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumatatu, Machi 27, 2017.
Juma la 4 la Kwaresima
Isa 65: 17-21;
Zab 29: 2, 4-6, 11-13;
Yn 4: 43-54.
IMANI KWA YESU
Leo, tunamwona Jemedari
anamwomba Yesu kwa ajili ya uhai wa mtoto wake. Anaweka Imani kamili kabisa kwa
Yesu. Anadhihirisha Imani yake kwa Yesu. Wakati Yesu alivyosema “waweza kwenda,
mtoto wako yu mzima” bila hata kupoteza dakika moja huyu Jemedari anaondoka.
Hili linaonesha Imani yake kamili kwa Yesu. Baada ya Yesu kusema mtoto wa huyu
Jemedari alipona. Huyu jemedari anashuhudia muujiza. Anapokea kadiri ya Imani
yake.
Kitu cha kuvutia cha kugundua
katika Injili hii ni utofauti wa maneno ya Yesu. Kwanza kabisa, inaonekana kama
Yesu amekasirika aliposema, “bila watu kuona ishara na miujiza, hamuamini”.
Lakini mara moja anamponya kijana wa jemedari kwa kumwambia, “Mwanao atakuwa
mzima”. Je, kwanini kuna utufatui katika maeneno haya ya Yesu na matendo yake?
Yesu anatambua kwamba watu wengi wana Imani dhaifu. Antambua pia ishara na
miujiza inasaidia watu wakati mwingine waweze kuamini. Lakini kilele cha
malengo ya Yesu haikuwa kwa sababu ya kuponya mwili.
Leo hii dunia imetawaliwa na
ugonjwa wa kimwili, kisaikologia na kiroho. Watu wanaenda kutoka sehemu moja
hadi nyingine kwenda kutafuta msaada. Lakini je, tunaenda kwa Yesu yeye ambaye
ni mponyaji wa Kimungu, ambaye haponyi tu mwili bali roho pia? Je, tuna Imani
kama huyu jemedari?
Sala: Bwana, tafadhali ongeza Imani
yangu. Ninakuomba nikuone wewe ukitenda katika maisha yangu, na nisaidie niweze
kutambua upendo wako mkamilifu kwa kila kitu. Ninapo kuona wewe ukitenda katika
maisha yangu, nisaidie niweze kuutambua kwa hakika kabisa, upendo wakomkamilifu.
Amina.
0 blogger-facebook:
Post a Comment