“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumatatu, Machi 6, 2017.
Juma la 1 la Kwaresima
Law 19: 1-2, 11-18;
Zab 19: 8-10, 15;
Mt 25: 31- 46
NI NANI NDUGU YANGU ALIYE MDOGO?
Kwaresima ni kipindi cha kufanya yote upya, kubadili tabia zetu na kufanya mazuri zaidi na kuacha mabaya. Ni mwaliko wakwenda juu zaidi ya mtizamo wetu wa kawaida wa kibinadamu wakutazama vitu na kuangalia maisha yote na uhusiano na wengine, kwa jicho la Mungu. Mara nyingi tunajitizama wenyewe na tunadhani kwamba sisi ni watakatifu, kwasababu hatutendi dhambi kama wengine. Lakini leo tunaitwa tuende mbele zaidi ya hilo, tukuwe katika fadhila na neema.
Injili ya leo inatuambia kwamba, Yesu atatuuliza yote tulio watendea walio wadogo kwamba tuli mlinitendea Yeye. Ni ajabu kwamba Yesu anaonesha kabisa kwa kusema kwamba ni watu wadogo, pengine wale wanao onekana ni wadhambi kabisa, walio dhaifu, walio wagonjwa, wasio jiweza walio na njaa na wasio na makao, na wote wale wanao shindwa kupata mahitaji ya maisha. Jambo nzuri kabisa Yesu anajitambulisha mwenyewe kuwa na wanyonge, wadogo wa aina zote. Kwa kuwatumikia walio na mahitaji ya pekee tunakuwa tuna mtumikia Yesu. Na kwa kuonyesha muungano na wao namna hiyo, Yesu anafunua utu wao kama wanadamu.
Tutafakari juu ya utu wa kila mtu. Je, unaangalia nini kwa huyo mtu? Ni kitu ghani unakitumia kumhukumu? Ni ndani ya huyu mtu, ambapo Yesu anatusubiria sisi. Anatusubiri sisi tuweze kumpenda yeye kwa walio dhaifu na wanao onekana hawafai. Tujitoe wenyewe kuwapenda na kuwatumikia , kwani ndani yao tutampenda na kumtumikia Bwana.
Sala: Bwana mpendwa, ninaelewa na kuamini wewe upo, katika hali ya kujificha kwa walio wanyonge na dhaifu, masikini na katika wadhambi walio kati yetu. Ninaomba nikutafute wewe kwa kila mmoja nitakaye kutana naye, hasa wale walio wahitaji. Yesu nakuamini wewe. Amina.
Tabia Takatifu ya Kwaresima-HESHIMA-Bwana nisaidie mimi nijifunze tabia ya HESHIMA. Ninaomba niwaheshimu watu wote kwa utu kabisa. Amina.
0 blogger-facebook:
Post a Comment