Na. James Waibina.
Mpenzi msomaji wa Jarida la Fumbuka na BLOG yetu ya Fumbuka, Nichukue fursa hii ya pekee kukukaribisha katika makala hii ya Ndoa na Mahusiano, makala ambayo hukuletea mafundisho mbalimbali kwa wanandoa na
kwa wale wanaotarajia kuingia katika Agano hilo.
Leo katika makala hii, ninakuletea maana na umuhimu wa zawadi kwa wanandoa.
Moja ya kitu ambacho huwa
hakina kipaumbele sana katika mahusiano ya kimapenzi ni zawadi. Lakini ukweli ni kwamba zawadi ina maana kubwa
sana katika mahusiano ya kimapenzi zaidi hata kuliko udhaniavyo.
Na Katika tafiti ambazo
zimewahi fanywa ni kwamba suala zima la utoaji zawadi katika mahusiano ya
kimapenzi limekuwa likileta hisia zaidi katika upande mmoja. Yaani hapa nikiwa
na maana ya kwamba jinsia ya kike ndiyo ambayo ipo katika kusubiri zawadi
kutoka kwa jinsia ya kiume. Kutoka na suala hilo ndo maana watu wengi wamekuwa
hawatilii maanani suala zima la zawadi. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu
anahusika kutoa zawadi.
Kujua zawadi ambayo mwenzi
wako anapendezwa nayo ni jambo la msingi sana, Unachotakiwa kukifanya ni
kwamba kwa kuwa mpenzi wako ni mtu wa karibu sana kwako, jaribu kuchunguza ni kitu gani ambacho
huwa anakipendelea sana.
Baada ya kupata majibu anza
kufanya uchunguzi mwingine ni kitu gani ambacho huwa anapenda kukizungumzia sana, baada
ya kupata majibu, majibu hayo yaweke katika halmashauri yako ya kumbukumbu. Na
mwisho wa siku mnunulie kitu hicho kwani ndiyo zawadi itakayompendeza.
Hayo ni baadhi ya mambo
machache ya kuzingatia katika kufanya uchaguzi wa zawadi ya kumpa mpenzi wako.
Kwani zawadi ni ishara ya upendo imara. Pia inashauriwa kwamba zawadi ni heri iwe ya
kudumu kwani hii hukumbukwa daima.
Pasipo kupoteza muda
tuendelee kidogo kwa kuangalia japo kwa uchache umuhimu wa zawadi katika
mahusiano ya ndoa.
1.Huimarisha uhusiano na
kuongezeka mapenzi ya kweli.
Pindi utoapo zawadi kwa
mwenzi wako, mwenzi huyo hujihisi yeye ni wa thamani sana mbele yako. Kwani
zawadi kutafsiriwa na mpokeaji kama ni mtu wa thamani sana, mtu ambaye
anapendwa kweli. Hivyo pindi ufanyapo kitendo cha utoaji wa zawadi
yeyote ile kwa mwenzi wako, hufanya mahusiano yenu yaimarike na si
kuteteleka.
2. Humfanya mtu
ajihisi yupo mahali salama.
Usishangae huo ndio ukweli,
kama ulikuwa hauna kawaida ya kumpa zawadi mpenzi wako basi anza kufanya hivyo
mara moja. Kwani zawadi hutafsiwa na mpokeaji ya kwamba yupo mahali
sahihi. Hivyo ili kuweza kuudumisha upendo wako na mwenzi wako jenga utaratibu
wa kumpa zawadi mpenzi wako.
3. Zawadi huacha
kumbukumbu.
Hakuna kitu ambacho huacha
alama kubwa katika mahusiano kama zawadi. Hivi hajawahi kukutana na mtu
anamwambia ya kwamba kitu hiki alinipa fulani? Bila shaka umewahi
kukutana na mtu wa aina hiyo. Kama ndivyo hivyo amini ya kwamba zawadi
huacha alama katika mahusiano.
Na ili kuacha alama hiyo,
kama nilivyosema hapo awali ua kwamba zawadi ni lazima iwe ni ya kudumu. Pia
kabla sijaweka nukta nikumbushe pande zote mbili kila mmoja ana haki ya kutoa
zawadi kwa mwezi wake. Hivyo nikusihi ya kwamba ujijengee utaratibu wa kutoa
zawadi kwa mwezi wako.
******************************************************************************************************
0 blogger-facebook:
Post a Comment