SOMO 1
Yer.
17:5-10
Bwana asema hivi: Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye
mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake, na moyoni mwake amemwacha
Bwana. Maana atakuwa kama fukara nyikani, hataona yatakapotokea mema; bali
atakaa jangwani palipo na ukame, katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, ambaye
Bwana ni tumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, uenezao
mizizi yake karibu na mto; hautaona hofu wakati wa hari ujapo, bali jani lake
litakuwa bichi; wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, wala hautaacha
kuzaa matunda.
Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una
ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? Mimi, Bwana, nauchunguza moyo,
navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya
matendo yake.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA
KATIKATI
Zab.
1:1-4, 6 (K) 40:4
(K) Heri aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake.
Heri mtu yule asiyekwenda
Katika shauri la wasio haki;
Wala hakusimama katika njia ya wakosaji;
Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo,
Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. (K)
Naye atakuwa kama mti uliopandwa
Kandokando ya vijito vya maji,
Uzaao matunda yake kwa majira yake,
Wala jani lake halinyauki;
Na kila alitendalo litafanikiwa. (K)
Sivyo walivyo wasio haki;
Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
Kw akuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki,
Bali njia ya wasio haki itapotea. (K)
SHANGILIO
Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia,
Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako.
INJILI
Lk.
16:19-31
Yesu aliwaambia Mafarisayo: Palikuwa na mtu mmoja,
tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa
anasa. Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda
vingi, naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza
ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. Ikawa yule maskini
alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye
akafa, akazikwa.
Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika
mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema,
Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini,
auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu
akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika
maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa
anafarijiwa, na wewe unaumizwa. Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi
kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala
watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa
baba yangu, kwa kuwaninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao piawakafika
mahali hapa pa mateso. Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize
wao. Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea atokaye kwa wafu,
watatubu. Akamwambia wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu
akifufuka katika wafu.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
0 blogger-facebook:
Post a Comment