MWANZO:
Zab. 27:8 – 9
Moyo wangu umekuambia, Bwana, uso wako
nitautafuta. Usinifiche uso wako.
SOMO 1
Mwa. 12:1 – 4a
Bwana akamwambia Abrahamu, Toka wewe
katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi
nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na
kulitukuza jina lako; nawe uwe Baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye
akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Basi Abramu akaenda, kama Bwana
alivyomwamuru.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 33:4 – 5, 18 – 20, 22 (K) 22
(K) Ee Bwana, fadhili zako zikae nasi,
Kama vile tulivyokungoja Wewe.
Kwa kuwa neno la Bwana lina adili,
Na kazi yake yote huitenda kwa
uaminifu.
Huzipenda haki na hukumu,
Nchi imejaa fadhili za Bwana. (K)
Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao,
Wazingojeao fadhili zake.
Yeye huwaponya nafsi zao na mauti,
Na kuwahuisha wakati wa njaa. (K)
Nafsi zetu zinamngoja Bwana;
Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.
Ee Bwana, fadhili zako zikae nasi,
Kama vile tulivyokungoja Wewe. (K)
SOMO 2
2Tim. 1:8b – 10
Uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili
ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu; ambaye alituokoa akatuita kwa mwito
mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake
yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele, na
sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili
mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO
Mt. 17:5
Sauti ya Baba ilitoka katika wingu
jeupe: “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, msikieni yeye.”
INJILI
Mt. 17:1 – 9
Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na
Yohane nduguye, akawaleta juu yam lima mrefu faraghani; akageuka sura yake
mbele yao; uso wake ukang’aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru. Na
tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye.
Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana,
ni vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka, nitafanya hapa vibanda vitatu, kimoja
chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya.
Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu
jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema,
Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye. Na wale
wanafunzi waliposikia, walianguka kifulifuli, wakaogopa sana.
Yesu akaja, akawagusa, akasema,
Inukeni, wala msiogope. Wakainua macho mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema,
Msimwambie mtu yeyote habari ya maono hayo, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka
katika wafu.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
0 blogger-facebook:
Post a Comment