MWANZO
Isa. 66:10 – 11
Furahi, Jerusalemu,
mshangilieni ninyi nyote mmpendao; furahini, ninyi nyote mliao kwa ajili yake,
mpate kunyonya, na kushibishwa kwa maziwa ya faraja zake.
SOMO 1
1Sam. 16:1b, 6 – 7, 10 – 13a
Bwana akamwambia
Samweli, Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese,
Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe.
Ikawa walipokuja, Samweli
alimtazama Eliabu, akasema, Yakini masihi wa Bwana yupo hapa mbele zake. Lakini
Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa
maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana
wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo.
Yese akawapitisha
wanawe saba mbele ya Samweli, Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa.
Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema,
Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia
Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku. Basi
akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na
umbu lake lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana
huyu ndiye.
Ndipo Samweli
akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya
Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
ZAB. 23 (k) 1
(K) Bwana ndiye
mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
Bwana ndiye
mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na
kitu.
Katika malisho ya
majani mabichi hunilaza,
Kando ya maji ya
utulivu huniongoza. (K)
Hunihuisha nafsi
yangu; na kuniongoza
Katika njia za haki
kwa ajili ya jina lake.
Naam, nijapopita
kati ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa mabaya;
Kwa maana Wewe upo
pamoja nami,
Gongo lako na fimbo
yako vyanifariji. (K)
Waandaa meza mbele
yangu,
Machoni pa watesi
wangu.
Umenipaka mafuta
kichwani pangu,
Na kikombe changu
kinafurika. (K)
Hakika wema na
fadhili zitanifuata
Siku zote za maisha
yangu;
Nami nitakaa
nyumbani mwa Bwana milele. (K)
SOMO 2
Efe. 5:8 – 14
Zamani ninyi mlikuwa
giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru; Kwa
kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli; mkihakiki ni nini
impendezayo Bwana. Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali
myakemee; kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena. Lakini
yote yaliyokemewa hudhihirishwa na nuru; maana kila kilichodhihirika ni nuru.
Hivyo husema, Amka wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO
Yn. 8:12
Mimi ndimi nuru ya
ulimwengu, asema Bwana, yeye anifuataye atakuwa na nuru ya uzima.
INJILI
Yn. 9:1 – 41
Yesu alipokuwa
akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi wake wakamwuliza
wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata
azaliwe kipofu? Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali
kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake. Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye
aliyenipeleka maadamu ni mchana; usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi. Muda
nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu.
Alipokwisha kusema
hayo alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za
macho, akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake,
Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona.
Basi jirani zake, na
wale waliomwona zamani kuwa ni mwombaji, wakasema, Je! Huyu siye yule aliyekuwa
akiketi na kuomba? wengine wakasema, Ndiye. Wengine wakasema, La; lakini
amefanana naye. Yeye mwenyewe alisema, Mimi ndiye.
Basi wakamwambia,
Macho yako yalifumbuliwaje? Yeye akajibu, Mtu yule aitwaye Yesu alifanya tope,
akanipaka macho akaniambia, Nenda Siloamu ukanawe; basi nikaenda na kunawa,
naikapata kuona. Wakamwambia Yuko wapi huyo? Akasema, Mimi sijui.
Basi wakampeleka kwa
Mafarisayo yule aliyekuwa kipofu zamani. Nayo ilikuwa sabato, hapo Yesu alipofanya
zile tope na kumfumbua macho. Basi Mafarisayo nao wakawmuliza tena jinasi gani
alivyopata kuona. Akawaambia, Alinitia tope juu ya macho, nami nikanawa, na
sasa naona. Basi baadhi ya Mafarisayo wakasema, Mtu huyo hakutoka kwa Mungu,
kwa sababu haishiki sabato. Wengine wakasema, Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya
ishara kama hizo? Kukawa matengano kati yao. Basi wakamwambia yule kipofu mara
ya pili, Wewe wasemaje katika habari zake kwa vile alivyokufumbua macho?
Akasema, Ni nabii.
Basi Wayahudi
hawakusadiki habari zake, ya kuwa alikuwa kipofu, kisha akapata kuona; hata
walipowaita wazazi wake yule aliyepata kuona. Wakawauliza wakisema, Huyu ndiye
mwana wenu, ambaye mnasema kwamba alizaliwa kipofu? Amepataje, basi, kuona
sasa? Wazazi wake wakawajibu, wakasema, Tunajua ya kuwa huyu ndiye mwana wetu,
tena ya kuwa alizaliwa kipofu; lakini jinsi aonavyo sasa hatujui; wala hatujui
ni nani aliyemfumbua macho. Mwulizeni yeye mwenyewe; yeye ni mtu mzima;
atajisemea mwenyewe. Wazazi wake waliyasema hayo kwa sababu waliwaogopa
Wayahudi; kwa maana Wayaahudi walikuwa wamekwisha kuafikiana kwamba mtu
akimkiri kuwa ni Kristo, atatengwa na sinagogi. Ndiyo sababu wale wazazi wake
walisema, Ni mtu mzima, mwulizeni yeye.
Basi mara ya pili
wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu, wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi
tunajua ya kuwa mtu huyo ni mwenye dhambi. Basi yule mtu akajibu, Kwamba yeye
ni mwenye dhambi sijui. Najua neno moja, kuwa mimi nilikuwa kipofu na sasa
naona. Basi wakamwambia, Alitutendea nini? Alikufumbua macho jinsi gani?
Akawajibu, Nimekwisha kuwaambia, wala hamkusikia; mbona mnataka kusikia tena?
Ninyi nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake? Basi wakamshutumu, wakasema, Wewe u
mwanafunzi wake yule; sisi tu wanafunzi wa Musa. Sisi tunajua ya kuwa Mungu
alisema na Musa; bali yule hatujui atokako. Yule mtu akajibu, akawaambia, Hili
ni ajabu! Kwamba ninyi hamjui atokako, naye alinifumbua macho! Twajua ya kuwa
Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi
yake; humsikia huyo. Tokea hapo haijasikiwa ya kuwa mtu ameyafumbua macho ya
kipofu, ambaye alizaliwa hali hiyo. Kama huyo asingalitoka kwa Mungu,
asingeweza kutenda neno lolote.
Wakajibu,
wakamwambia, Ama! Wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufundisha sisi?
Wakamtoa nje. Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe
wamwamini Mwana wa Mungu? Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate
kumwamini? Yesu akamwambia, Umemwona, naye anayesema nawe ndiye. Akasema,
Naamini, Bwana. Akamsujudia.
Yesu akasema, Mimi
nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe
vipofu. Baadhi ya Mafarisayo waliokuwapo pamoja naye wakasikia hayo,
wakamwambia, Je! Sisi nasi tu vipofu? Yesu akamwambia, Kama mngekuwa vipofu,
msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Kristo
0 blogger-facebook:
Post a Comment