“KWARESIMA
YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima, Jumatano,
Machi 22, 2017.
Juma la 3 la Mwaka wa
Kanisa
Masomo:
Kumb 4:1, 5-9
Zab 147: 12-13,15-16,19-20;
Mt 5:17-19
YESU:
UTIMILIFU WA SHERIA
Masomo ya leo yanatupa
picha kuhusu sheria ya Mungu. Ni za taratibu na kamilifu. Yesu alifanya kurejea
“sheria na Manabii” akisema kwamba hakuja kutengua sheria za manabii bali
kuzitimiza. Zilikuja kutimizwa baada ya miaka elfu na zaidi. Ilichukuwa muda kwa
utimilifu wa mpango wa Mungu kujifunua. Lakini ulijifungua kwa wakati wake na
kwa jinsi yake. Ni hakika, wale wote waliokuwa katika Kipindi cha Agano la Kale
walikuwa na shauku ya Masiha kuja ili kutimiza vitu vyote. Nabii baada ya nabii
alikuja akinyoosha kidole mbele kwa wakati ujao kwamba Masiha atakuja. Hata
sheria za Agano la Kale katika hali Fulani zilikuwa ni kwa ajili ya kuwaandaa
watu wa Mungu kwa ajili ya ujio wa Masiha. Lakini ilikuwa ni hali ya taratibu
ya kutengeneza sheria, kuziweka kwa watu wa Israeli, kuwasaidia ili kuzielewa,
na kuanza kuziishi. Hata Masiha alivyokuja, kuna wengine kwasababu ya shauku na
furaha walitaka atimize yote kwa wakati mmoja. Walitaka Ufalme wao wa dunia
uanzishwe na walitaka Masiha wao mpya achukue Ufalme wake.
Lakini mpango wa Mungu ni
tofauti kabisa na hekima ya Binadamu. Njia zake zilikuwa tofauti kabisa na njia
zetu. Na njia zake zikaendelea kuwa mbali kabisa na njia zetu! Yesu alitimiza
kila sheria katika Agano la Kale na Manabii, na si kama vile watu walivyokuwa
wanadhani. Wayahudi wakati wa Yesu walikuwa wamejikita mno katika sheria
binafsi na mapokeo katika sheria ya Musa kiasi kwamba walipoteza picha halisi.
Iliwawia vigumu kumtambua Yesu kwamba yeye mwenyewe ndiye mtimilifu wa sheria,
kwamba alikuwa sheria ya Mungu iliochukuwa umwilisho. Kwa maneno yake na
matendo yake alileta sheria katika maisha. Sio tena mlolongo wa Maandishi,
sheria sasa zilikuwa kitu cha kuishi katika uhalisia na kila mtu alihisi.
Tafakari kwa kujitafiti mwenyewe kama nawe ni mtu wa kuangalia tu karibu kama
Wayahudi! Je, unamuona Yesu kama anayeishi na mtilifu wa sheria?
Sala:
Bwana, ninakabidhi maisha yangu kwako. Nina amini kwamba una mpango kamili
kwangu na kwa watoto wako wapendwa. Nipe subira niweze kukusubiri wewe na
nikuache wewe ulete mapenzi yako ya Kimungu yatimie katika maisha yangu. Yesu
nakuamini wewe. Amina
Tabia Takatifu ya
kwaresima: KUISHI KAMA KRISTO-Ee Mungu nisaidie niweze kuishi kama Yesu
alivyoishi kwani yeye ndiye utimilifu wa sheria zote. Nifanye niweze kuishi
kama Mwanao ili niwalete wote kwako. Amina
0 blogger-facebook:
Post a Comment