728x90 AdSpace

­
Latest News
March 3, 2017

TAFAKARI YA KWARESIMA: Njaa kwa Ajili ya Mungu



“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Ijumaa, Machi 3, 2017,
Ijumaa baada ya Jumatano ya majivu

Isa 58: 1-9;
Zab 51: 3-6, 18-19;
Mk 9: 14-15.

NJAA KWA AJILI YA MUNGU!

“Muda utafika wakati Bwana harusi ataondolewa kwao, ndipo watafunga” (Mt 9:15). Tunaitwa wote kuwa na njaa kwa ajili ya Mungu na ufalme wake. Kufunga kunatusaidia. Yesu analinganisha ujio wa Ufalme wa Mungu ambao aliutangaza na kuuanzisha, na sherehe ya harusi ya Wayahudi. Kufunga wakati wa harusi ingekuwa ajabu kabisa. Kutakuwa na muda wa kufunga baada ya Yesu kuondoka kati ya Wafuasi wake, na kuwaachia wanafunzi wake kazi ya kuukamilisha ufalme wake. Tupo katika kipindi cha kwaresima. Kama Yesu alivyoenda jangwani kufunga na kusali alivyo anza kazi yake ya kutangaza na kuusimika Ufalme wa Mungu, pia tunapaswa kumwomba Mungu neema ya pekee kwa kufunga na kusali tukiwa tunaendelea na kazi ya kuutangaza Ufalme wa Mungu duniani.

Isaya anatueleza mambo muhimu ya kufunga. Kufunga ina hali ya wima na hali ya mlalo (Wima –kwa ajili ya Mungu, mlalo-kwenda kwa wanadamu). Kwanza kabisa, ni kazi ya mtu binafsi, kwa ajili ya mapendo ya Mungu. Tunatoa sadaka si kwasababu ya ukosefu wa chakula, bali tunatoa sadaka kwa vile tunavyo vipenda, ili tuweze kukuwa kwa mapendo kumwelekea Mungu. Pili, hakuna mfungo ulio na matunda mazuri isipokuwa kwa ajili kujali jirani. Tusipo punguza makali ya wale walio wagonjwa, walio na njaa, waliotengwa, tusipokuwa sauti ya wajane, sauti ya Yatima, mfungo wetu hautakuwa na sauti mbele za Mungu. Hivyo, angalao tujifunze kazi moja ya matendo ya huruma, kwa kuwashirikisha yote tunayo jinyima na wale wahitaji. Kwa kufunga chakula tunajifunza ni kwa jinsi ghani njaa inavyouma, na hivyo kuwa na huruma daima kwa wale ambao tunasikia kwamba wana njaa. Hatufungi ili kujilimbikizia kwa baadae bali ili tuwasaidie kile tulichofunga, na isiwe tu baada ya kuwasaidia inakuwa mwisho, bali kwasababu tutakuwa tumejifunza ni kwajinsi ghani njaa inauma, itufanye tuwafikirie daima wale wanao kosa chakula kila wakati. Siku za Ijumaa wakati wa kwaresima ni siku ambazo Kanisa pia linatuhimiza kufanya kitubio. Kitu muhimu katika ijumaa za kipindi cha Kwaresima inapaswa kuwa siku ya majitoleo.

Sala
Bwana, ninachagua siku hii, ili niweze kuwa wamoja pamoja na wewe, katika mateso. Ninaomba majitoleo na matendo yangu ya kujikatalia ninayo kutolea, yawe chanzo cha muunganiko wa ndani pamoja na wewe. Yesu nakuamini wewe. Amina.

Tabia Takatifu wakati wa Kwaresima. KUFUNGA-Bwana nisaidie mimi nijifunze tabia ya KUFUNGA. Ninakuomba niwe mkarimu kwa kile nilicho nacho kwa ajili ya wengine. Amina.

Copyright ©Fumbuka BLOG.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: TAFAKARI YA KWARESIMA: Njaa kwa Ajili ya Mungu Rating: 5 Reviewed By: Unknown