"KWARESIMA YA UKARAIMU”
Tafakari ya kwaresima
Jumatatu, Machi 20, 2017.
Juma la 3 la Kwaresima
Sherehe ya Mt. Yosefu, Mume wa Bikira
Maria.
2Sam 7:4-5,12-14,16;
Zab 89:2-5,27,29;
Rum 4:13,16-18,22;
Mt 1:16,18-21,24 au Lk 2:41-51
Mt. YOSEFU: MTU WA NDOTO NA MTU WA
KAZI!
“Wakati Yosefu alivyo amka, alifanya
kama malaika alivyo mwambia” (Mt 1:24). Haya maneno ya mwisho ya Injili ya leo,
yanatupa muktasari mzima wa sherehe ya leo, ya Mt. Yosefu mume wa Bikira Maria.
Maandiko yanatuambia kuwa Yosefu alikuwa mwana wa Yakobo na mume wa Maria na
pia ni Mseremala kutoka Nazareth. Baada ya kumposa Maria, baada ya kutambua
Bikira Maria ana mimba kabla hawajaanza kuishi pamoja, Yosefu akiwa ni mtu
mwaminifu katika sheria, anaacha kumwaibisha Maria na ana azimu kumwacha kwa
siri. Mungu aliongea naye kwenye ndoto na akatii. Malaika wa Bwana alimtokea
katika ndoto na akafunua mpango wa Mungu kwa mwanadamu, na akamchukua Maria
nyumbani kama mke wake.
Cha kuvutia, ni kwamba Yosefu hajaongea
neno lolote katika maandiko (Injili). Bali ni mtu wa vitendo tu: anafanya
alicho ambiwa na Malaika, anamchukua Maria kama mke wake na anaenda Bethlehemu:
anatafuta sehemu ya kujihifadhi usiku, na anachukua familia yake Misri.
Ingawaje sio matu wa maneno, lakini kwa hakika ni mtu wa matendo. Mungu alikuwa
na mpango na Yosefu, na alikuwa tayari kuyafanya mapenzi ya Mungu. Alikuwa ni
mtu ambaye alikuwa akiyafuata mapenzi ya Mungu. Shauku ya maisha ya baadae, na
vipingamizi vya nje havikumzuia kuacha kuyatimiza mapenzi ya Mungu. Kwasababu
alikuwa mwamini fu kutimiza mapenzi ya Mungu, Mungu alikuwa naye katika maisha
yake yote.
Somo la kwanza kutoka katika kitabu cha
Samueli na pia wimbo wa katikati unatumbia kwamba Mfalme Daudi aliahidiwa kuwa
mtoto wake ataishi milele. Daudi hakubaki mpaka kuiona ahadi hii ikitimia.
Katika somo la pili, Paulo anawaeleza Warumi kuhusu Abraham, mtu mwingine
mwenye haki ambaye hakuishi mpaka kuona matunda ya kazi yake. Alifanya mapenzi
ya Mungu, lakini hakuona kutimia kwa ahadi ya Mungu kwake. Ingawaje
hayakutimizwa kwa kipindi chake alitumaini na kuamini na Imani yake ilimpa
kibali kwa Mungu. Katika somo la Injili tunamuona Yosefu mwenye Imani kwa
Bwana. Alitembea katika majaribu mbali mbali kwa Imani. Aliamka kutoka katika
ndoto na anakaanza kuweka kwenye matendo. Nini tunaweza kujifunza kutoka kwa
Yosefu.
Utii kwa Mungu zaidi kuliko mwanadamu:
sheria ilimwambia Yosefu kumwacha Maria na kumwacha aadhibiwe. Lakini
hakusikiliza mawazo yake mwenyewe au kilichosemwa na sheria na watu. Yeye kwa
nafsi yake anafuata mapenzi ya Mungu. Yosefu alikuwa mtu shujaa katika kumtii
Mungu licha ya msukumo wa tamaduni. Je, jamii au Imani yangu inaleta mchango
katika maamuzi yangu?
Wito ni muhimu kuliko kazi zetu: kwa
Yosefu mpango wa Mungu maishani mwake ulikuwa muhimu zaidi kuliko mambo yake ya
kijamii, kazi na familia. Yosefu yeye alikuwa Baba mume kabla yakuwa mseremala.
Mungu wake, na familia yake ilikuwa muhimu zaidi kuliko kazi yake. Wito wake
ulipita kazi zake. Je, familia yangu inakuwa muhimu zaidi kuliko kazi yangu?
Familia inapaswa kuwa ya kwanza.
Mlinzi wa nyumba yake: Yosefu alikuwa
mtu wa kuwa karibu na mke wake na kulinda familia yake. Anaitwa pia mlishi na
mlinzi wa kanisa Katoliki. Watu walio mfano wa Yosefu ndio tunaokosa siku hizi.
Watoto wetu wana achwa na kuingia kwenye hatari kama, mitandao, picha chafu,
ulevi nk. Je, ni kwa jinsi ghani tulivyo walinzi wa familia zetu?
Mtu wa vitendo: Yosefu alikuwa
mfanyakazi, na Mseremala. Hakuwa tu mtu wa ndoto, alikuwa mtu mchapa kazi,
aliyepata chakula chake kwa uaminifu. Yosefu ni mfano kwetu kwa watu wanaopata
chakula chao kwa kufanya kazi kihalali.
Yosefu ni mlinzi na mlishi wa Kanisa
Katoliki, mlinzi na mlishi wa kanisa katika hatua za mwanzo, wakati kanisa
lilipokuwa, Yesu, Maria na Yosefu. Tunafanya vizuri kumuiga Mt. Yosefu na
kumuomba atuombee kama akina Baba wa familia walishi na walinzi. Mt. Yosefu
utuombee..
Sala: Bwana, tunakuomba tuwe watu
wakuiga maisha ya Mt. Yosefu ili tuweze kuwa tayari kutimiza mapenzi yako bila
kuwa na wasi wasi. Yesu nakumini wewe. Amina
Tabia Takatifu ya Kwaresima: KUFANYA
KAZI- Bwana nisaidie niweze kuwa mtu wa kufanya kazi kama Mt. Yosefu. Ninaomba
nisitumie njia za kifupi, bali mpango wako na mapenzi yako kwangu. Amina
0 blogger-facebook:
Post a Comment