Utangulizi
Katika
Kalenda ya Kanisa Katoliki, huwa mwezi wa tano na mwezi wa kumi ni miezi ambayo
imewekwa kwa ajili ya Bikira Maria na Mama Kanisa. Hivyo hiyo miezi huwa
inasaliwa rozari. Wengi waweza kujiuliza kuwa ni kwa nini ifanyike miezi hiyo?
Yafuatayo ni majibu, mwezi wa tano umewekwa kwa heshima ya Bikira Maria
kutokana na nini kilitokea katika historia hapo nyuma. Mnamo Karne ya 16 mwezi
watano kwa miaka yote ulikuwa ni mwezi ambao sikukuu nyingi za kiserikali ndo
zilikuwa zikifanyika. Kanisa kwa kutambua hilo nalo likahidhinisha pia mwezi wa
tano uwe ni mwezi wa Rozari, na kwa makusudi zaidi Kanisa lililenga kuwa
sherehe hizo ziendane na taratibu za wakristu, ni kwa msingi huo sherehe hizo
ziliendana na mwezi wa rozari na kutokea hapo ikahidhinishwa kuwa mwezi wa tano
wa mwaka ni mwezi wa Bikira Maria. Pia mwezi wa kumi (October) pia ni mwezi wa
Bikira Maria na pia ni mwezi wa Kusali Rozari kutokana na historia ya hapo
nyuma pia, na ilikuwa kwamba baada ya ushindi wakristo walioupata katika vita
baina yao na yule aliyeitwa Lepanto mnamo 7 October, 1571, Papa wa wakati ule
Papa Pius V aliufanya huo ushindi kuwa ulitokana na maombezi ya Bikira Maria,
na alisema kuwa rozari ni silaha kubwa hata kuliko silaha kubwa za kivita. Ni
Kwa msingi huu tunaona kuanzia hapo mwezi wa kumi ukawa mwezi uliotengwa na
Mama Kanisa kwa Bikira Maria, na pia ukaitwa mwezi wa Rozari.
Historia yenyewe
Ni kwamba
sala ya Rozari inasemekana kuanzishwa na Mt. Dominico aliyezaliwa mnamo mwaka
1170 na kufariki mwaka 1221 na hiyo sala Mt. Dominico aliipata kwa njia ya
ufunuo ambapo Bikira Maria alimtokea na kumwamuru awe anasali rozari. Bikira
Maria alimwamuru mtakatifu Dominico kusali rozari kwa kipindi hicho iwe kama
silaha yake ili kupambana na uzushi uliokuwa umeibuka ukipingana na mafundisho
ya Kanisa, na huo uzushi uliitwa ‘ Albigensia’ hili ni kundi lilokuwa na imani
kuwa Duniani kuna nguvu nguvu mbili zenye uwiano sawa lakini hupingana na
kupigana moja baada ya nyingine, nazo nguvu hizo ni Mungu na Shetani. Hivyo
hawa waliamini kabisa kuwa Mungu na Shetani wana nguvu sawa ( Dualistic )
waliamini pia kuwa dunia hii imejaa uovu kwa kuwa iliumbwa na mwovu. Ni kwa
msingi huu Kanisa liliamua kupambana na hawa wazushi ambao pia walionekana
kupotosha mafundisho ya Kanisa. Ndipo tunaona Bikira Maria anamtokea Mtakatifu
Dominico na kumwambia asali rozari ili kupambana na mafundisho hayo ya kizushi.
Ni Papa Pio V ambaye mnamo mwaka 1569 alihidhinisha rasmi kusali rozari kwa
kanisa nzima na kuhidhinisha rozari iwe jinsi tunavyoiona sasa. Katika zile
zama za kati, watawa wamonaki walizoea kusali zaburi 150, na kwa upande wa
waumini walei ambao kwa kipindi hicho hawakujua kusoma zaburi iliwabidi wasali
sala ya Baba yetu mara 150 baadala ya zaburi 150 na hizo baba yetu walizisali
kwa kuhesabu punje 150 zilizokuwa zimefungwa kwenye kamba ndefu ambayo kwa
lugha ya kitaalamu iliitwa “ Corona” au kwa Kiingereza “ Crown” kadiri ibada
kwa Bikira Maria ilivyoendelea kushamiri mnamo Karne ya 12, sala kwa Bikira
Maria ilianzishwa na hivyo kuanza kusali salamu maria 150 baadala ya baba yetu
150.
Salamu
Maria 150 hapo baadaye zilikuja kugawanywa katika makundi/ mafungu na Mtawa
mdominica aliyeitwa Henry Kalkar ( 1328-1408), ambapo kila tendo la rozari
lilikuwa na mafungu 50 ya salamu Maria ambapo pia kila fungu liligusia maisha
ya Bikira Maria na Yesu katika historia ya wokovu wetu. Zaidi ya hapo, mtawa
mwingine wa mdominican aliyeitwa Alanus de Rupe aliendelea kugawanya hiyo
historia ya matendo ya wokovu wetu katika matendo ya furaha,uchungu, na
utukufukama tunavyoyaona sasa. (NB Matendo ya mwanga hayo ni ya majuzi siyo ya
wakati ule). Na nikuanzia hapo Bikira Maria amepewa nafasi kubwa katika shirika
la watawa wa Dominican. Hivyo utamaduni wa kusali rozari umeendelea karne hata
karne, mfano Papa Leo XIII (1878-1903) aliweka msisitizo mkubwa juu ya ibada ya
rozari kwa Bikira Maria. Kuanzia September 1, 1883 Baba Mtakatifu Leo XIII
aliandika jumla ya barua za kichungaji 11 zote zikiwa zinaweka mkazo juu ya
rozari. Hivyo rozari ni sala inayotokana na maandiko matakatifu( Biblia).
Mafumbo ya rozari yote yanapatikana katika agano jipya ambapo ndo tunaona
matendo ya Bikira Maria na Yesu Kristo katika wokovu wetu.
tunakumbushwa
uchungu aliopata Bikira Maria Katika maisha yake hasa ule utabiri wa Simeoni
kwa Bikira Maria juu ya mateso na kifo cha mwanae Yesu, Matendo saba ya furaha
kwa Maria ambapo yaananza na kupashwa habari kwa Bikira Maria na Malaika wa
Bwana, kupalizwa mbinguni, na matendo ya huruma ya Bikira Maria kwa wale ambao
wanaendelea kuteseka hapa duniani.
0 blogger-facebook:
Post a Comment