“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya kwaresima
Ijumaa, Machi 10, 2017,
Juma la 1 la Kwaresima
Eze 18:21-28;
Zab 130: 1-8;
Mt 5:20-26.
KUWA MWEMA!
Leo, Nabii Ezekieli anaweka mbele yetu matarajio ya Mungu kwetu sisi. Anatoa sura ya Mungu akiwa amejawa na huruma kwa wale wote ambao hutubu dhambi zao. Hata hivyo anamuonesha Mungu akiwa hakimu wa haki aliye mwema asiye pendezwa na mabaya. Mungu hataki mtu aliye katika pande mbili (anayechanganya mema na mabaya kwa wakati mmoja), yeye anatazama kila mmoja wetu katika nafsi nzima.
Katika Injili Yesu anaongelea kuhusu Ufalme wa Mbinguni. Kuingia katika Ufalme wa mbinguni unapaswa kuwa lengo la Maisha yetu. Ni mara nyingi tunashindwa kuliona hili katika maisha. Tunashindwa kufungua macho yetu kuelekea Mbinguni kama lengo letu la kwanza la kuwa hapa duniani. Ni rahisi kunaswa na kuridhika na hali za kila siku kama viburudisho, pesa, mafanikio, na mengineyo.
Yesu anatupa njia ya pekee ya kufuata katika ujumbe huu wa Injili, jinsi ya kupata lengo la maisha-ufalme wa Mbinguni. Njia anayo ionesha ni haki. Haki maana yake ni kuwa mwaminifu, sio mdanganyifu. Mafarisayo walijifanya kwa kujionesha kuwa walikuwa watakatifu na wafuasi wazuri wa mapenzi ya Mungu. Lakini hawakuwa wazuri katika hilo. Wanaweza kuwa wazuri katika hali ya kutenda na huenda wanaweza kuwa wamewavutia watu, lakini hawakuweza kumdanganya Yesu. Yesu aliweza kuona udanganyifu wao na kujificha kwao kusiko kwakweli na akaona kile kilicho jificha. Yesu aliweza kuona haki yao ni kwa ajili tu ya kujionesha wenyewe kwa watu.
Kama tunataka kufanya Mbingu kuwa lengo letu, tunapaswa kujitahidi kuwa watakatifu. Na waaminifu. Tunapaswa kumtafuta Kristo katika hali ya kweli na uaminifu katika vitu vidogo vya maisha. Tunapaswa kuacha uaminifu huo uweze kungaa kwa kuonesha katika kweli kile kilichopo katika hali ya ndani. Kuwa wenye haki katika hali ya kweli, ni kwamba tunamtafuta Yesu katika hali ya haki na kumfanya Mungu kuwa lengo la maisha yetu.
Sala: Bwana, naomba unifanye mwenye haki. Nisaidie niweze kuwa mwaminifu kwa yote ninayofanya na yote ninayo tafuta katika maisha. Nisaidie mimi nikupende wewe kila wakati na siku zote. Yesu, nakuamini wewe. Amina
Tabia Takatifu ya Kwaresima: HAKI-Bwana nisaidie mimi niweze kujifunza tabia ya HAKI, Ninaomba nisiwe mtu mnafiki bali mtu mwaminifu na mkweli. Amina.
0 blogger-facebook:
Post a Comment