SOMO 1
Isa. 1:10, 16-20
Lisikieni neno la Bwana, enyi waamuzi
wa Sodoma; tegeni masikio msikie sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora.
Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa
matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; achene kutenda mabaya; jifunzeni
kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima
haki yake; mteteeni mjane.
Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana.
Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa
nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya
nchi; bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha
Bwana kimenena haya.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 50:8-9, 16-17, 21, 23 (K) 23
(K) Autengenezaye mwenendo wake,
Nitamwonyesha wokovu wangu.
Sitakukemea kwa ajili ya dhabihu zako,
Na kafara zako ziko mbele yangu daima.
Sitatwaa ng’ombe katika nyumba yako,
Wala beberu katika mazizi yako. (K)
Una nini wewe kuitangaza sheria yangu,
Na kuliweka agano langu kinywani mwako?
Maana wewe umechukia maonyo,
Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.
(K)
Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza,
Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe,
Atoaye dhabihu za kushukuru, ndiye
anayenitukuza.
Naye autengenezaye mwenyendo wake,
Nitamwonyesha wokovu wa Mungu. (K)
SHANGILIO
Mt. 4:17
Tubuni asema Bwana, kwa maana ufalme wa
mbinguni umekaribia.
INJILI
Mt. 23:1-12
Yesu aliwaambia makutano na wanafunzi
wake, akasema, Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; basi,
yoyote watakayowaambia, myashike, na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo
yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi. Wao hufunga mizigo mizito na
kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao. Tena
matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupapanua hirizi
zao, huongeza matamvua yao; hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi
mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi.
Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu
wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu. Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba
yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni. Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni
mmoja, naye ndiye Kristo. Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. Na
yeyote atakayejikweza atadhiliwa; na yeyote atakayejidhili atakwezwa.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
0 blogger-facebook:
Post a Comment