“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya
Kwaresima
Ijumaa, Machi
24, 2017,
Juma la 3 la
Kwaresima
Hos 14:2-10;
Zab
81:6-11,14,17;
Mk 12:28-34
CHAGUA KUMPENDA MUNGU!
Mwandishi
alimuuliza Yesu, “ni amri ipi iliyokuu?” na Yesu akajibu ni “Upendo”. Upendo
tunao ufahamu na kuhisi katika maisha ni “hali ya kujisikia/kuhisi kutoka ndani
mwetu”; hisia, au hali ya kujisikia tunayo ilinganisha na vitu tulivyopokea au
kutamani. Katika hali fulani vitu na watu huongoza upendo wetu.
Lakini,
anachosema Yesu kuhusu “upendo” ni kitu kingine tofauti. Huu ni upendo ambao
tunaweza kuumudu, tunao amua kuutoa. Mungu haitaji upendo wetu ili yeye aweze
kuishi. Lakini ameamua kutupatia maisha. Hii si kwasababu anatuhitaji sisi,
bali kwasababu anapenda kuutoa. Hii ndio maana ya upendo wa Mungu usio na
masharti. Anachotaka Mungu kutoka kwetu ni kuchagua kumpenda yeye kama yeye
alivyo chagua kutupenda sisi. Na tunapo fanya hivyo tunapokea upendo wake
zaidi, kwani tunabaki katika upendo wake. Kwahiyo, leo tuchague kumpenda Mungu
kwa akili zetu zote, na hapo hatutakuwa mbali na ufalme wake.
Hatua ya
kwanza katika kumpenda Mungu ni kutaka kumfahamu. Hii ina maana tunapaswa
kutafuta jinsi ya kumfahamu, na kutaka kumuelewa na kumwamini Mungu na yote
yaliyo funuliwa kwetu kuhusu yeye. Ina maana tumeamua kujikita katika kuingia
kufahamu mafumbo ya maisha ya Mungu, hasa kwa njia ya Maandiko Matakatifu na
kwa njia ya ufunuo wa mafundisho ya Kanisa katika historia ya Kanisa. Pili,
tunaingia katika undani kwa kufuata njia zake. Jambo hili la uhuru kamili
linapaswa kufuata akili yetu kuhusu yeye na kuwa kitendo cha Imani kwake. Tatu,
tunapo ingia katika kutaka kuyaelewa mafumbo ya maisha ya Kimungu na kuchagua
kumwamini na yote aliyo tufunulia, tutaona maisha yetu yatabadilika. Njia
maalumu itakayo badilika ni kwamba tuta tamani kuwa na Mungu na kufanya mapenzi
yake katika maisha yetu, tuta tamani kumtafuta zaidi, tutapata furaha kwa
kumfuata na tuta tambua kuwa upendo wa roho yetu kama wanadamu utazama katika
upendo wake na katika njia yake. Tafakari ni mara ngapi umetamani kumfahamu
Yesu na kutaka kufahamu yote aliyo tufunulia.
Sala: Bwana, ninaomba niwe mwaminifu
katika kujikita kwangu ili niweze kukufahamu zaidi na kufahamu ukweli wa
utukufu wa maisha yako. Ninakushukuru kwa yote ulionifunulia mimi na
ninajitolea maisha yangu, leo, katika harakati za kufahamu maisha yako na
ufunuo wako. Yesu nakuamini wewe. Amina.
0 blogger-facebook:
Post a Comment