SOMO 1
Kumb. 4:1, 5-9
Musa aliwaambia makutano: Ee Israeli,
zisikilizeni amri na hukumu niwafundishazo, ili mmzitende; mpate kuishi na
kuingia na kuimiliki nchi awapayo Bwana, Mungu wa baba zenu.
Angalieni nimewafundisha amri na
hukumu, vile vile kama Bwana, Mungu wangu, alivyoniamuru, ili mzitende katika
nchi mwmingiayo ili kuimiliki. Zishikeni basi, mkazitende, maana hii ndiyo
hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa watakaozisikia amri hizi zote,
nao watasema, Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na akili. Kwa maana
liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama Bwana, Mungu
wetu, alivyo, kila tumwitapo? Tena liko taifa gani kubwa, lililo na amri na
hukumu zenye haki kama torati hii yote, ninayoiweka mbele yenu leo.
Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde
roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako,
yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako
na watoto wa watoto wako.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 147:12-13, 15-16, 19-20 (K) 12
(K) Msifu Bwana, Ee Yerusalemu.
Msifu Bwana, Ee Yerusalemu;
Msifu Mungu wako, Ee Sayuni.
Maana ameyakaza mapingo ya malango
yako,
Amewabariki wanao ndani yako. (K)
Huipeleka amri yake juu ya nchi,
Neno lake lapiga mbio sana.
Ndiye atoaye theluji kama sufu,
Huimwaga barafu yake kama majivu. (K)
Humhubiri Yakobo neno lake,
Na Israeli amri zake na hukumu zake.
Hakulitendea taifa lolote mambo kama
hayo,
Wala hukumu zake hawakuzijua. (K)
SHANGILIO
Mbegu neno la Mungu, mpanzi lakini ni Kristu; Yeyote ampataye, ataishi
milele.
INJILI
Mt. 5:17-19
Yesu aliwaambia wanafunzi wake:
Msidhani kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali
kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,
yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka hata yote yatimie. Basi mtu
yeyote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu
hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda
na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme mbinguni.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
0 blogger-facebook:
Post a Comment