“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumapili, Machi 5, 2017.
Jumapili ya 1 ya Kwaresima
Mwa 2:7-9; 3:1-7;
Zab 51:3-6, 12-14, 17;
Rum 5: 12-19;
Mt 4: 1-11.
VISHAWISHI-NAFASI YA KUKUWA!
Kushawishiwa , maana yake ni kuvutwa kwenye kitu kisichoruhusiwa. Injili ya Leo inatuambia Yesu alijaribiwa “Kristo kuhani Mkuu, alijaribiwa kwa kila namna kama tulivyo lakini hakutenda dhambi” (Ebr 4:15). Biblia inatualika tutazame vishawishi kama nafasi ya kujipima uchaguzi wetu, nafasi ya kukuwa. Uchaguzi upo kati ya kukubali mpango wa Mungu au kuukataa. Adamu aliamua kuchagua njia isiofaa/hukumu yake mwenyewe; Kristo daima alirejea neno la Mungu daima. Adamu alinyoosha mkono wake juu ya tunda la kifo; Yesu amekuwa chanzo cha uhai.
Kitabu cha Mwanzo kinamuonesha mwanadamu akiwa katika bustani ya Edeni, ambapo katikati yake kulikuwa na mti wa “uhai” na “maarifa” mema na mabaya. Ni kwa ajili ya Mungu na unawakilisha vizuizi viwili ambavyo havipaswi kuvukwa. Kwanza unawakilisha alama ya Mungu, mtoa uhai, na asiyeweza kufa. Mwanadamu kunyoosha mkono juu ya mti huu ni sawa na kukataa hali yake ya kibinadamu. Pia mti ni wa maarifa ya mema na mabaya. Kunyoosha mkono juu ya mti huu ni kutaka kuwa mkuu wa maamuzi yako na matendo yako mwenyewe. Ni jambo kubwa la kutaka kujianzilishia ukuu-kuanza kumpinga Mungu au kukataa maneno yake ya Kibaba ambayo ni maneno ya maadili mema ya kuchagua. Wakati mwanadamu anasahau kwamba yeye ni kiumbe aliyeumbwa na kujaribu kujifanya Mungu, mjuaji wa mema na mabaya anajimaliza mwenyewe. Ni wazi kwamba anaanza kuita “ubaya kuwa ni wema na kuita wema ni ubaya: kubadili giza kuwa mwanga na mwanga kuwa giza, vitu vichungu na kusema vitamu, au kusema vitamu kuwa vichungu” (Isa 5:20).
Nyoka anaingia katikati na anawaalika Adamu na Eva kula tunda lililokatazwa. Kitabu cha Hekima kinanyambulisha kuwa ni muovu. (Hek 2:23-24). Kinatufanye tushangae ni muovu yupi anaye shawishi na kudanganya. Nyoka ni mnyama , mwerevu kuliko wanyama wote aliyeumbwa na Mungu. Ni kilele cha kazi ya Mungu aliofanya. Ndio, nyoka si mwingine isipokuwa mwanadamu mwenyewe ambaye, kwa kufikia kilele cha majivuno yake, anatambua mwisho wa uwezo wake. Anajitengenezea maadili yake mwenyewe, akijifanya kutenda mambo katika hali ya kipekee. Nyoka anawakilisha hali yetu ya kupenda mapenzi yetu yawe zaidi ya mapenzi ya Mungu, kujiona wenyewe kuwa Mungu. Ndio sehemu hii ya mwanadamu inatufanya tutende pasipo Mungu. Maneno ya nyoka si kitu kingine zaidi ya mawazo yetu ya ndani ambayo ndipo dhambi inapo anzia. Kitu kingine ni dhambi. Dhambi inazaliwa kwa kutafuta vitu vizuri na vya furaha. Uharibifu ni kwamba, kutokumwamini Mungu, mwanadamu anachagua sehemu mbaya, kupoteza lengo na kujiangamiza mwenyewe. Baada ya dhambi hawaukubali ukweli. Wanajaribu kujificha na kujisikia kukata majani na kujifunika wenyewe.
Katika somo la pili, Paulo najaribu kuonesha kwamba Adamu ni wazi anajukumu la maovu yote. Anatumia ulinganishaji, kati ya Adamu na Kristo kuelezea kazi ya ukombozi alioitimiza Yesu. Adamu alitaka kuwa bwana wa mema na mabaya, na badala yake akapata kifo kama mshahara wake. Kristo, kinyume na Adamu, alitambua utegemezi wake na Mungu. Alikuwa daima mwaminifu kwa Baba, akawa Bwana wa uhai. Wote wanaomfuata na kuiga utii wake kwa Baba watafanywa wenye haki.
Katika somo la Injili, “Yesu alikaa jangwani kwa siku arobaini na alijaribiwa na shetani” (Mk 1:12-13). Kwa kutumia lugha ya Biblia na lugha ya picha, alimaanisha maisha yote ya Yesu yalikuwa kati yake na huku shetani akimjaribu. Majibu ya Yesu kwa shetani yanawakilisha matukio matatu ya wana Waisraeli katika kitabu cha kutoka: manunguniko ya chakula na zawadi ya manna (Kut 16), kugoma kwasababu ya maji (Kut 17), kuabudu ndama wa shaba (kut 32) hivyo Yesu anayaishi tena maisha ya watu wake. Yeye anapatwa na majaribu yale yale, lakini anayashinda. Ni wale tu, wanaothamini maisha yao katika mwanga wa neno la Mungu wanaoweza kutoa ushuhuda wa kweli Ulimwenguni.
Vishawishi vipo. Ni matokeo ya maanguko ya wanadamu wa kwanza. Yanatoka katika udhaifu wetu lakini pia kutoka katika yule muovu. Yesu hakukubali kuanguka katika vishawishi alivyokuwa jangwani na wala hakuanguka katika kishawishi katika maisha yake yote. Aliyashinda na kuteseka kwa ajili ya hayo. Hili linatuambia kwamba anaweza kuwa kiongozi wetu na mfano wetu wa kuiga wakati tukiwa katikati ya vishawishi kila mara na kila siku. Wakati mwingine tunaweza kujisikia wa pweke tuliotengwa katika jangwa la dhambi zetu. Tunaweza kujisikia kama vile mnyama mkali wa tamaa zetu unatushinda. Tunaweza kujisikia yule muovu anatunyemelea. Sawa, Yesu alipatwa na haya pia. Aliruhusu kupitia haya kwa kushiriki ubinadamu wetu. Kwa njia hii ni Yesu anayeweza kukutana nasi katika jangwa letu. Yupo tayari anatusubiri, akitutafuta, akituita sisi. Ni huyu alieyeshinda vishawishi vya muovu jangwani, ndiye atakaye tuongoza kuepuka. Kwahiyo, kama jangwa lako ni mahangaiko ya maisha sasa, au ni majaribu mbali mbali, Yesu anataka kukutana nawe akuongoze katika njia iliyo njema. Alimshinda yule wa jangwani na jinsi alivyokuwa, hivyo anauwezo wakushinda jangwa lolote lile katika maisha yako.
Sala: Bwana, ninakubali upendo wako mkamilifu kwangu. Nina amini kwamba unanipenda mimi kiasi kwamba nitaweza kuvumilia mateso, kuelewa mateso yote. Ninakuomba nikutane nawe katika jangwa la maisha yangu. Ninakuomba nikuruhusu wewe uniongoza katika sehemu tulivu na yenye maji. Yesu nakuamini wewe. Amina
0 blogger-facebook:
Post a Comment