“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumamosi, Machi 4, 2017,
Jumamosi baada ya Jumatano ya majivu
Isa 58: 9-14;
Zab 86: 1-6;
Lk 5: 27-32
KUMTEMBELEA DAKTARI YA MIOYO YETU!
Roho ya kweli ya Kwaresima ni, kufunga, kutoa sadaka na sala, yote haya yamejengwa juu ya kwenda kinyume na matamanio yetu, na kutamani kuwa na Mungu katika Ufalme wake. Hii haina maana kwamba mmoja anapaswa kuacha kwa muda wa siku 40 ili awasaidie maskini wakati wa Kwaresima tu. Tunapaswa kuelewa nafasi mbali mbali zinazokuja katika maisha yetu ya kila siku. Ni muda pia wa kuacha dhambi na kupokea uponyaji kutoka kwa mganga mtakatifu.
Yesu aliwahitaji wadhambi. Yeye ni mkombozi, na mkombozi aliwahitaji wadhambi ili awakomboe! Kuja kwa Yesu tukiwa na mizigo ya dhambi zetu, inampa furaha katika moyo wake. Anafurahi kwasababu anatimiza ule utume aliotumwa na Baba yake, akionesha kuruma yake kama Mkombozi pekee. Muacha akupe huruma yake! Unafanya hivi kwa kuja kwake katika hali yako ya dhambi na kujinyenyekesha mbele kama asiestahili huruma yake, na ambaye unastahili tu hukumu. Kuja kwa Yesu inamfanya yeye aweze kuonesha huruma yake kutoka katika chemchemi ya huruma yake.
Angalia katika hali ya kwamba Yesu ni Mganga Mtakatifu anayekusubiri ili aweze kutimiza wajibu wake wa kuponya. Anakuhitaji wewe ukubali dhambi zako na kuwa wazi kwa uponyaji wake. Kwa kufanya hivyo, unaruhusu mlango wa huruma yake ufunguke na kumimina baraka kwako na katika kipindi chetu.
Sala: Mpendwa Mkombozi na Mganga Mtakatifu, ninakushukuru kwa kuja kutukomboa na kutuponya. Ninakushukuru kwa tamaa yako ya kuonesha huruma yako katika maisha yangu. Naomba uninyenyekeshe niweze kuwa wazi kwa uponyaji wako. Yesu nakuamini wewe. Amina
Tabia takatifu ya Kwaresima: kutembelea wagonjwa-Bwana nisaidie mimi niweze kuwa na tabia ya kutembelea wagonjwa hospitalini, nyumba za wazee na jirani zangu. Ninaomba niwe chanzo cha uponyaji ili waweze kupokea uponyaji wako.
0 blogger-facebook:
Post a Comment