Na. James J. Waibina
Mpendwa
msomaji wa Jarida letu la Fumbuka na BLOG yetu ya Fumbuka kupitia fumbukasasa.blogspot.com Nichukue fursa hii ya pekee kukukaribisha katika
makala hii ya FAHAMU, makala ambayo hukufahamisha masuala mbalimbali yahusuyo
maisha na jamii yetu kwa ujumla.
Leo
katika Makala hii ninakuletea Dalili za mtu aliyekata tamaa katika Jambo lolote
maishani mwake hivyo karibu uwe nami ili uweze kujifunza mengi yamkini nawe
umekata tamaa ila hujijui.
Awali
ya yote ni vyema tukafahamu maana ya kukata tamaa..
MAANA YA KUKATA TAMAA
Kukata
tamaa ni hali ya kupoteza matumaini, hari hii hutokea pale ambapo mtu amepoteza
wazo au matumaini ya kufanikiwa katika matarajio yake ya kupata kitu fulani au
kufanikiwa kwa jambo lolote alilopanga.
Pia
ni kupoteza tumaini la kufikia malengo katika jambo fulani alilopanga kulifanya
au analolifanya, ni hali inayoweza kutokea katika mfumo wa maisha ya kila siku,
iwe nyumbani, Kazini, shuleni, kwenye biashara, katika mahusiano au mahali
pengine popote katika mfumo wa maisha.
Hii
ni hali ya kuchoshwa au kuvunjwa moyo kunakotokana na mtazamo hasi unaoweza
kuujenga baada ya kufikia Ukomo wa ufahamu, ufumbuzi au suluhisho la
suala lolote linalokukabili, iwe kutokana na mawazo yako binafsi au mawazo ya
yatokanayo na wengine.
Hili
ni tatizo kubwa linalowafanya watu kutofikia malengo yao au kutopata mafanikio
katika maisha yao ya kila siku.
Baada
ya kuangalia Maana ya Kukata tamaa, sasa
tuangalie dalili za mtu aliyekata tamaa.
Kuna
dalili nyingi za mtu aliyekata tamaa ambazo hutofautiana kutokana na mazingira,
sababu, wahusika, matukio n.k.
Lakini
zipo dalili za msingi na za jumla kwa watu wote. Dalili hizo tunaweza kuzigawa
katika sehemu Kuu mbili ambazo ni:
(i) Dalili za Ndani
Hizi
ni dalili ambazo watu wengine nje ya mhusika hawawezi kuzitambua kiurahisi, ni
muhusika tu ndiye anaweza kuzitambua au kuhisi.
(ii)
Dalili za Nje
Hizi
ni dalili ambazo watu wengine nje ya mhusika tunaweza kuwa mashahidi kwa
kuziona kwa uwazi na kutambua kwamba mwenzetu amekata tamaa.
Sasa
tuziangalie dalili hizi angalau kwa undani zaidi.
DALILI ZA NDANI ZA MTU ALIYEKATA
TAMAA
1. Kukosa msukumo kimawazo.
Kwakua
kila jambo linaanzia kwenye mawazo, ili mtu afanikiwe anahitaji msukumo na
ushawishi wa mawazo yake.
Maana
mawazo anayokuwanayo mtu kwa muda mrefu, huwa yanajitokeza katika maneno yake
na hatimaye katika matendo yake.
Hivyo
basi ukiona msukumo wa mawazo yako ya mwanzo umepungua, basi ujue kuwa hiyo ni
dalili mojawapo ya kukata tamaa.
2.
Kuhisi kuchoshwa kimawazo
Ukiona
mawazo yako yamechoshwa kwa kuliwazia jambo fulani ambalo mwanzoni ulikuwa
umelipanga vizuri, nayo ni dalili ya kukata tamaa.
Kwa
leo tuishie hapo.....
*****************************************
*****************************************
ITAENDELEA
........
Imetayarishwa
na: James J. Waibina
Kwa
Maoni /Ushauri: Tuwasiliane kupitia
0713515059 -(WhatsApp)
au
MBARIKIWE.
0 blogger-facebook:
Post a Comment