Na. James Waibina.
Habari ndugu msomaji
wa makala zangu katika blog hii ya Fumbuka, karibu tena siku ya leo tuweze
kujifunza zaidi kuhusu Ndoa na Mahusiano, leo tutazungumzia umuhimu wa kuwa
katika ndoa kwa upande wa uchumi na afya.
Ndoa ni muunganiko wa watu wawili wenye nia ya kuishi pamoja kwa maisha yao yote. Ni muungano wenye malengo ya kujenga familia pamoja na kuiongoza kwa namna ambavyo itakuwa bora kwao kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.
Utafiti unaonyesha kuwa kuna faida za kuwa katika ndoa kiuchumi na kiafya.
Watu walio katika
ndoa huwa na afya njema na pia huwa na maendeleo zaidi kiuchumi ukilinganisha
na wale ambao wanaishi peke yao.
Hali kadhalika
wananafasi kubwa ya kufanya mambo makubwa zaidi ya maendeleo kuliko watu wawili
ambao hawako katika ndoa.
Hii inasababishwa na
mtindo wa maisha ambao wasio katika ndoa wanaishi, vitu kama ulaji mbaya,ulevi
usio na mipaka na matumizi mabaya ya fedha zao.
Faida za Kiafya za Kuwa Katika
Ndoa.
Kwa wastani utafiti
unaonyesha watu ambao wako katika ndoa wanaishi maisha marefu yenye afya na
furaha zaidi kuliko wale wasiokuwa katika uhusiano wa ndoa.
Wanaume ambao hawana
uhusiano wa ndoa wanakawaida ya kula vibaya vyakula visivyo na faida kiafya,
baadhi yao wanakuwa walevi na matumizi yao ya fedha yanakuwa makubwa. Kwa
kuwa hawapiki nyumbani, hula sehemu za jumuia kama migahawani na katika vilabu
vya pombe. Vyakula hivi havina mchanganyiko mzuri wa virutubisho
vinavyohitajika katika mwili.
Wanawake wasioolewa
nao ulaji wao wakati mwingi unakuwa wa kula nje japo si kama wanaume, lakini
pia wanakula vibaya vyakula vyenye mafuta mengi na visivyo na virutubisho
muhimu. Vyote katika hivi vinapelekea kuhatarisha afya zao lakini pia wakati
mwingine maandalizi ya vyakula hivyo huwa si mazuri.
Wanawake na wanaume
ambao wameachana au mwenza wao amefariki wanasongwa sana na upweke wa kihisia.
Hili hupelekea kupata magonjwa yanayosababishwa na msongo wa mawazo.
Faida za Kiuchumi za Kuwa Katika
Ndoa.
Kuna faida nyingi
zinazotokana na watu kuwa katika ndoa ambazo huleta mafanikio kiuchumi, faida
hizo ni miongoni mwa;-
i. Matumizi Machache:
Tumeona kuwa watu wasiokuwa katika ndoa hula chakula nje zaidi na kunywa vilevi, hivyo hutumia fedha zaidi kwa mambo yasiyo ya msingi hasa kwa wanaume. Wanawake hali kadharika hutumia fedha nyingi katika mavazi na vipodozi wakiwa hawako katika ndoa kuliko wale walioolewa.

ii. Malengo ya Muda
Mrefu:
Mipango ya watu wasio katika ndoa huwa ni ya muda mfupi na starehe zaidi hivyo kufanya maendeleo yao kiuchumi kuwa chini. Kinyume chake ni kuwa wale ambao wako katika mahusiano hupunguza matumizi kwa kula nyumbani zaidi na kupunguza matumizi katika vitu visivyo vya muhimu kama mavazi ya fahari.

Malengo ya watu
waliooana huwa ya kujenga familia na ni malengo ya muda mrefu. Badala ya
kufanya starehe kupita kiasi huwekeza katika ujenzi na biashara ambazo
zitaongeza kipato chao.
iii. Kipato Kikubwa:
Kipato chao pia huongezeka kwa kuweka nguvu pamoja. Kama wote ni waajiriwa basi kutakuwa na mishahara miwili mwisho wa kila mwezi badala ya mtu mmoja na hivyo uwezo wao wa kufanya mambo makubwa unaongezeka.

Watoto wanapozaliwa
katika familia huongeza mahitaji ya familia na ghrama huongezeka. Kwa kuwa
inasemekana kuwa “uwezo wa binadamu kufikiri hukua kutokana na tatizo” wazazi
walio katika ndoa hupata jinsi nyingine ya kuongeza kipato na hivyo kukua
kiuchumi. Watafikiria miradi zaidi au hata kutafuta kazi inayowalipa zaidi.
Hitimisho:
Ni wazi kuwa kuna
raha ya kuwa na mtu unayempenda katika maisha yako na kujenga naye familia.
Kama ndoa yenu ina furaha ni wazi utakuwa mtu mwenye furaha; na inajulikana
kuwa mtu mwenye furaha huishi maisha marefu na huwa na afya nyema.
Hali kadhalika walio
katika ndoa wana wajibika zaidi kuliko wale wasio katika ndoa na huweka
jitihada za ziada za kujiongezea kipato. Hivyo uchumi wa walio katika ndoa
huimarika zaidi na kuwafanya waendelee kwa haraka.
Lakini ifahamike
kuwa hili linawezekana tu kama ndoa yao ina furaha, ikiwa vinginevyo matokeo
huwa kinyume chake.
Nashukuru kwa kuwa nami katika makala hii.
Kwa maoni au ushauri wowote usisite kuniandikia kupitia
0713 515059 -Text/Call/ WhatsApp
jameswaibina@fumbuka.co.tz -email.
Nashukuru kwa kuwa nami katika makala hii.
Kwa maoni au ushauri wowote usisite kuniandikia kupitia
0713 515059 -Text/Call/ WhatsApp
jameswaibina@fumbuka.co.tz -email.
0 blogger-facebook:
Post a Comment