728x90 AdSpace

­
Latest News

Fumbuka BLOG ni sehemu ya Jarida la FUMBUKA ambayo hutoa habari na makala mbalimbali zilizomo katika jarida hilo kwa njia ya Mtandao.

Katika BLOG hii utajifunza mambo mengi yanayohusu Imani, Jamii, Habari za Kanisa, MafundIsho mbalimbali, Masomo katika Biblia, Nyimbo za Injili, Wasifu wa watu mbalimbali n.k

Hivyo nyote mnakaribishwa sana katika kujifunza na kufaidi mambo kadha wa kadha toka humu.

JARIDA LA FUMBUKA.
FUMBUKA ni Jarida litakalokufumbua akili kutoka katika Giza na kuwa katika Nuru yaani kukufanya Ufahamu na kuelewa masuala mbalimbali yahusuyo Imani, Jamii, Fursa mbalimbali pamoja na kukujuza mengi usiyoyajua. 

Jarida hili huandaliwa na Umoja wa Vijana Wakatoliki (VIWAWA) Parokia ya Pugu, Jimbo kuu la Dar es Salaam chini ya kampuni yao iitwayo Fumbuka Company ambayo lengo lake kubwa ni kuwasaidia na kuwainua vijana kiuchumi.

Makala za Fumbuka:
Jarida la FUMBUKA lina makala zilizoandaliwa na waandishi mahiri waliobobea katika tasnia hiyo wakiwemo Mapadri. 

Makala hizo zimegawanyika katika sehemu nne ambazo ni Makala za Imani, Jamii, Fahamu na Fursa kama ifuatavyo;-

1. Makala za Imani ni pamoja na;-
Kasisi Exclusive, Katekesi, Biblia ni Jibu, Historia ya Imani, Agape na Parokia.

2. Makala za Jamii ni pamoja na:-
Mwanamke Shujaa, Kijana Amka, Mtoto ni Malezi, Darasa la Ndoa na Afya Imara.

3. Makala za Fahamu ni pamoja na:-
Bustani ya Edeni, Fahamu,  Nyayo za Kale, Kwetu Kwao na Siwa.

4. Makala za Fursa ni pamoja na:-
Kilimo Pesa, Talanta Zetu,  Fursa kwa Wote, Lugha ya Muziki na Simulizi.

Uhariri:
Jarida hili lina bodi ya wahariri inayoongozwa na Mhariri Mkuu ambao huchunguza, kupitia na kurekebisha makala zote kabla hazijachapwa katika toleo husika la Jarida la Fumbuka.

************************************************

Kwa maoni au ushauri naomba uwasiliane na Mhusika wa blog hii kwa niaba ya timu nzima ya FUMBUKA kupitia:

Simu:  +255 713 515059 – (WhatsApp)
     +255 767 515059


Facebook: James Waibina

Mwanzilishi wa Blog hii anaitwa James Waibina, ambaye ndiye Mtaalamu wa IT wa FUMBUKA. Lengo na dhumuni la kuanzisha Blog hii ni kusaidia jamii hasa katika masuala ya Imani hususani IMANI MOJA KATOLOKI YA MITUME na pia lengo kuu zaidi ni kuelimishana na kufumbuana sisi sote katika masuala mbalimbali yanayoendelea ulimwenguni.

Hivyo kwa lolote lile ambalo unahisi linafaa kulingana na maudhui ya Blog hii usisite kutuma au kuwasiliana nasi kwa  anuani tajwa hapo juu.

Ahsante.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
Item Reviewed: Rating: 5 Reviewed By: Unknown