Jumatatu 13 Machi 2017 leo, Baba Mtakatifu
anatimiza miaka 4 tangu achaguliwe kuliongoza Kanisa Katoliki la Mungu na
katika tukio hili Kardinali Gerard Nichols ameandika Barua ya kumpongeza Baba
Mtakatifu Francisko katika utume huo wa Khalifa wa mtume Petro. Barua hiyo
inasema “tunamshukuru Mungu kwa utajiri wa zawadi na matunda ya Roho Mtakatifu,
ambayo ndiyo yameongoza tabia ya utume wa Papa Francisko yaani furaha ,
amani, uvumilivu , ukarimu , uaminifu , hekima na huruma.
Kardinali Nicholas
ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu wa Uingereza na Gales anamshukuru
sana Baba Mtakatifu kwa namna anavyojionesha , katika maneno , na matendo yake,
katika mafundisho yake ya Kristo na Kanisa, anaongeza Kardinali Nichols “
mafundisho hayo yanaambatana na uhai na pia kueleweka haraka na hata kuleta mvuto
kwa walio wengi duniani.Anasema, tumwombee ili Mungu aweze kumpatia nguvu
na ujasiri wa kuendelea na utume katika kiti cha Mtakatifu Petro.
Ikumbukwe kwamba,
Baba Mtakatifu Francisko alichaguliwa tarehe 13 Machi 2013, akiwa mfuasi wa 265
wa Mtume Petro. Aliingia madarakani mwezi mmoja wa kihistoria wa Kanisa
Katoliki mara baada ya kung’atuka kwa Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita.
Jioni ya tarehe 13 Machi Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita alikuwa
amemwambia yeye mwenyewe kwamba; tuanze safari hii ya uaskofu na watu: Safari
hiyo ya Kanisa la Roma, ambayo inatoa upendo kwa makanisa yote ya ulimwengu.
Safari ya undugu na upendo na kwa matumaini katika Yesu. Tuombe kwa ajili yetu
na kwa ajili ya wengine.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili
ya Radio Vatican.
0 blogger-facebook:
Post a Comment