Na. James Waibina.
Karibu Mpenzi Msomaji na mfuatiliaji wa Makala zetu katika Blog hii ya Fumbuka..
Baada ya kuangalia mbinu za kukusaidia kuwa mbunifu katika makala iliyopita, Leo katika Makala hii ya "Fursa kwa wote" ninakuletea Faida azipatazo Mtu aliye mbunifu katika biashara yake.
Ebu kwanza tujikumbushe maana ya Ubunifu, Ubunifu ni uwezo wa kuvumbua bidhaa au huduma mpya au mbinu mpya za namna ya kukamilisha jambo fulani kwa ufanisi, au tunaweza kusema ubunifu ni ujuzi wa kuleta jambo lilelile kwa muonekano tofauti.
Ebu kwanza tujikumbushe maana ya Ubunifu, Ubunifu ni uwezo wa kuvumbua bidhaa au huduma mpya au mbinu mpya za namna ya kukamilisha jambo fulani kwa ufanisi, au tunaweza kusema ubunifu ni ujuzi wa kuleta jambo lilelile kwa muonekano tofauti.
Ili uweze
kufanikiwa kwenye biashara yako unahitajika uwe mbunifu sana, yani hakikisha
leo yako ni tofauti na jana yako, kuwa mbunifu kila iitwapo leo kwenye biashara
yako utafanikiwa sana, unaweza kuwa unafanya biashara sawa na watu wengine
lakini kama wewe utakuwa mbunifu utaileta kwa muonekano tofauti ambao
utawafanya watu wengi wakupende wewe,kuwa mbunifu kwenye biashara yako
kutakuhakikishia mafanikio makubwa sana kwenye biashara yako.
Faida azipatazo mtu aliye Mbunifu katika biashara ni pamoja na;-
1. Kuongeza Uwezo
Mtu ambae
ni mbunifu siku zote yeye huumiza kichwa sana kuhakikisha kuwa anakuja na kitu
tofauti, hii humjengea uwezo mkubwa sana kwenye mambo yake, hivyo basi mtu
mbunifu ana uwezo mkubwa sana kwenye biashara zake kuliko mtu ambae sio mbunifu
kwasababu mtu mbunifu muda wote kichwa kinachakarika kuleta mawazo mapya.
2. Kuwa tofauti na wengine
Faida ya
kuwa mbunifu kwenye biashara yako ni kuwa tofauti na watu wengine. Siku zote
kwenye maisha hauwezi kuwa sawa na wengine kama wewe ni mbunifu kuliko watu
wengine, utakuwa watofauti tu hata kama watu watasema nini kuhusu wewe lakini
mwisho wa siku wewe utaendelea kuwa mtu wa tofauti tu kwenye maisha yako, kiuchumi,
kifikra na hata kimawazo kwa sababu ya ubunifu wako.
3. Kupunguza Ushindani
Kama tunavyojua
kuwa washindani ni wengi sana kwenye biashara yoyote ile, unachotakiwa
kuwashinda washindani wako sio kugombana nao, sio kuwatukana hapana
unachotakiwa kufanya hapo ni kuhakikisha wewe unakuwa mbunifu tu sana kwenye
biashara yako, jinsi unavyokuwa mbunifu ndio unazidi kuwapunguza, kwasababu wao
watajua kesho utakuwa vile vile kumbe kesho unakuja kivingine mwisho wa siku
utawaacha mbali tu kimaisha kwasababu wewe ni mbunifu kuliko wao.
4. Kuongeza Masoko
Faida nngineyi
ya kuwa mbunifu ni kuhakikisha unapata masoko sana, nilishakwambia hapo mwanzo
kuwa moja ya kitu kinachoweza kukufanya kupata masoko ni kuwa tofauti na huwezi
kuwa tofauti kama sio mbunifu, jitahidi sana kwenye maisha yako, kuwa mbunifu
utaona utakavyweza kupata masoko mengi ya kuuza bidha zako.
Hizo ndizo Faida azipatazo Mtu aliye Mbunifu katika biashara yake.
Ahsante.
Ahsante.
Kwa Maoni /Ushauri: Tuwasiliane kupitia
0713515059 -(WhatsApp) au jameswaibina@fumbuka.co.tz
0 blogger-facebook:
Post a Comment