728x90 AdSpace

­
Latest News
March 10, 2017

Pata Elimu ya kutosha kuhusu "Hisa" na Namna ya Kumiliki hisa katika Kampuni.


Na. James Waibina.

Watu wengi wamekuwa wakitamani kufanya biashara au shughuli yoyote ambayo itakuza kipato chao, lakini wengi wao hukatishwa tamaa jinsi gani ataweza kusimamia biashara hiyo.

Changamoto ya usimamizi wa biashara ni kubwa sana kwa watu wengi hasa wale ambao ni wafanyakazi serikalini na kampuni binafsi.
Na wengi ambao wamejaribu kufanya biashara wameshindwa kutokana na usimamizi mbovu wa biashara zao. Wengi wanatamani kukuza vipato kwa njia nyingine.

Uwekezaji katika hisa ni suluhisho kwa wale wote ambao wanakutana na changamoto ya muda wa usimamizi wa biashara zao. Uwekezaji katika hisa ni rahisi, unahitaji muda mdogo wa usimamizi, unakua na kuongeza kipato kwa mwekezaji.

Yawezekana wengi hawafahamu kuhusu Hisa, Umuhimu wake na vitu vya kuzingatia kabla ya kununua hisa, mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa makala zetu katika Blog yetu ya Fumbuka karibu katika makala hii tuweze kujifunza hayo.

Nini Maana ya Hisa?

Wengi miongoni mwetu wamekuwa wakitaka kujua HISA ni nini, shauku hii imenifanya nidodose kidogo juu ya hisa kwa faida ya wengi. Kwa tafsiri lahisi HISA NI UMILIKI.

Kwa kifupi kuwa na hisa ni kumiliki sehemu ya kampuni au kuwa mmiliki wa kampuni hiyo kwa maana hiyo unakuwa na nafasi ya kushiriki kufanya maamuzi, kupata faida au hasara katika kampuni hiyo.

Mtu akisema nina hisa NMB anamaanisha ana miliki NMB. Umiliki huu unajionyesha wazi na bayana wakati wa kufanya maamuzi na kugawana gawio (faida inayopatikana katika kampuni). Mwenye hisa nyingi huwa na sauti au ushawishi mkubwa katika kufanya maamuzi na hupewa gawio kubwa kwa uwiano wa hisa zake.

Mfano- Kampuni yaweza kuwa na hisa 1000, ikaamua kuuza hisa 500 na hisa 500 zikabaki akiba. Wale watakaonunua hizo hisa 500, wanakuwa wametoa mtaji kwa kampuni na kwa maana hiyo ndio wamiliki. Mwenye kuweza kununua hisa 251 atakuwa amenunua hisa nyingi zaidi kuliko yeyote na anakuwa na nguvu ya maamuzi katika vikao na gawio atapata kubwa kwa sababu ndie aliechangia mtaji mkubwa.

Nawezaje Kununua Hisa Katika Soko la Hisa?

Unaweza kununua hisa katika soko la Hisa la Dar es salaam kupitia mawakala wake (Brockers) au kupitia Benki ya CRDB ukiwa mkoa wowote ule hapa Tanzania.  

Unaweza pata taarifa zaidi kupitia website ya soko la hisa la Dar es salaam www.dse.co.tz

Wasiliana wakala utapata utaratibu wowote jinsi ya kununua hisa. Unachotakiwa kuwa nacho ni pesa yako kwa ajili ya kununua hisa, akaunti yako ya benki na mawasiliano ya Mawakala wa soko la Hisa au Benki ya CRDB.

Mambo gani ya kuzingatia kabla ya Kununua Hisa?

Kabla ya kununua hisa ni vyema ukaangalia mambo yafuatayo;

1. Performance ya kampuni.

Kampuni kama inafanya kazi vizuri kwa weledi na inamategemeo ya ukuaji wa kampuni hiyo kama kutanua matawi, kuongeza product au kukua kwa biashara katika kampuni hiyo basi hiyo ni kampuni nzuri.

Mfano;- Ukisikia kampuni imetanua soko lake kama CRDB ilivyofungua matawi nchi za nje inamaana ya kuwa faida ya kampuni hiyo itaongezeka na hivyo gawio linaweza kuwa kubwa na wewe kupata faida na pia bei ya hisa itaweza kuongezeka hivyo utapata faida pia pindi ukiamua uza hisa zako.

2. Bei ya hisa na uimara wake (stable share price)

Kuna kampuni ambazo bei zao za hisa wakati wote ni nzuri kwa maana hazishuki sana au mara kwa mara na pia zina tabia za kuongezeka mfano;- TBL, SWISS PORT, TCC.

3. Wakati wa kununua hisa

Ni muhimu pia kuangalia ni wakati gani unanunua hisa, mfano wakati ambao hisa ndio zinaingizwa au kuuzwa kwa mara ya kwanza kwenye soko la hisa bei huwa ni ndogo sana na baada ya hapo mara nyingi bei huongezeka ingawa kuna wakati hushuka pia.

Lakini bei ya hisa hupanda kushuka kutokana na nyakati katika mwaka mfano ifikapo mwishoni mwa mwaka na mwanzoni mwa mwaka bei hushuka na kuwa ndogo zaidi ila katikati ya mwaka bei huanza kupanda kwa kasi kubwa zaidi

4. Uwepo wa taarifa nzuri katika Kampuni.

Mfano imekuwa ikisikika kuwa benki ya CRDB itakuwa inatumika kulipia mishahara ya baadhi ya wafanyakazi wa serikali basi siku ukisikia imeingia mkataba huo au imeanza kutumika kulipia mishahara hiyo basi nenda kanunue hisa hizo haraka kwani bei ya hisa itaanza kupanda na pia gawio la faida litakuwa kubwa.

5. Wingi wa makampuni katika soko la hisa.

Mfano kuna mabenki zaidi ya matano hii inamaana benki hizi zinagombea wateja hii ni kwa wateja wote wale wanaowahudumia na wale wa kwenye soko la hisa hivyo bidhaa zao zipo za kutosha na bei itakuwa ya kawaida mambo ya demand na supply.

Kwa bei ya leo kampuni inayoongoza ni ACA-13200, TCC- 11500, TBL 11500, JHL 10900, SWISS 5400. Makampuni haya yote yanafanya shughuli tofauti na bei zake ni nzuri zaidi.

Napata Faida gani nikimiliki Hisa?

Zifuatazo ni Faida azipatazo Mtu anayemiliki Hisa katika Kampuni yoyote;-

1.   Gawio

Ukiwa miliki wa hisa utapata gawio ikiwa Kampuni itapata faida katika kipindi hicho cha mwaka na wanahisa wakaridhia utoaji wa gawio. Gawio hutolewa mara mbili au moja kwa mwaka kutokana sera ya kampuni na maamuzi ya wanahisa.

  2. Ongezeko la thamani

Wanahisa pia huweza kupata faida itokanayo na ongezeko la thamani iwapo bei ya hisa itaongezeka kwenye soko la hisa. Ikiwa ulinunua hisa moja kwa Tsh 800 na baada ya mwaka hisa hizo sokoni zikauzwa kwa Tsh 1,400 basi unakuwa umepata ongezeko la thamani ya shilingi 6,00 kwa kila hisa. Hii ni faida tofauti na gawio, ikiwa utawekeza katika kampuni nzuri utapata gawio na ongezeko la thamani ndani ya mwaka mmoja. 

Vile vile ikiwa bei itashuka na kufikia Tsh 600 utapata hasara ya Tsh 200. Ila ukiwekeza katika kampuni nzuri ni vigumu kupata hasara na unakuwa na uhakika wa bei kuongezeka kwa 20% au 40% au zaidi kwa mwaka.

  3. Dhamana

Hisa  kwa mwekezaji anaweza kuzitumia kama dhamana anapohitaji kupata mkopo.

4. Huokoa muda wa usimamizi

Ni uwekezaji ambao humpatia mwekezaji uhuru wa kufanya shughuli nyingine na kwa wale ambao hawana muda wa usimamizi katika biashara huu ni uwekezaji mzuri kwao.

5.   Ni mali inayohamishika kwa urahisi

Ni mali ambayo inahamishika ki urahisi na kwa haraka pale mwekezaji anapohitaji pesa yake kwa ajili ya shughuli nyingine.

6.   Akiba

Njia ya kujiwekea akiba kwa ajili ya baadaye.

7.   Ushiriki wa jamii katika Uchumi

Inasaidia kuongeza ushiriki wa jamii katika shughuli za kifedha na kukuza uchumi.

Napata Hasara gani nikimiliki Hisa?

Hasara ni pale unapokuwa na hisa chache kwani unakuwa kama unasindikiza wengine. Gawio unapata dogo na unakuwa huna ushawishi katika maamuzi. Hasara nyingine ni pale kampuni inapofanya vibaya, thamani ya hisa hupungua, waweza nunua hisa 1 kwa tsh 1000 ukauza 500 au hela zako zikazama. Ni vyema kupata ushauri wa kitaalamu kabla ya kununua HISA.

Natumaini umejifunza mengi kuhusiana na Hisa.

Mtu yoyote Yule anaweza kuwa mwanahisa akiwa popote pale Tanzania.
Ni uwekezaji ambao unaweza kuufanya ukiwa katika mkoa wowote ule hapa Tanzania kwa gharama ndogo na wewe kuwa mmiliki wa hisa na kutengeneza faida.

Ahsante.

Kwa Maoni /Ushauri: Tuwasiliane kupitia


0713515059  -(WhatsApp) au  jameswaibina@fumbuka.co.tz
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

22 blogger-facebook:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Well and good ... Asante kwa elimu ndugu

    ReplyDelete
  3. Asante kwa kutoa ulichonacho, nimefaha kitu angalau.

    ReplyDelete
  4. ahsante kwa funzo angalau nmeelewa kitu

    ReplyDelete
  5. Am u need more knowledge but thanks for a briefly explanation

    ReplyDelete
  6. Nimeelewa nini maana ya hisa na umiliki wa hisa

    ReplyDelete
  7. naomba kufaham pindi hisa zinaposhuka muwekezaji anapata hasara pindi atapouza kwa muda huo ???? au hasa asipouza hio hasara lazma imuhusu???

    ReplyDelete
  8. Ahsante Sana kwa elimu nzuri,,umetoa elimu Pana juu .ya hisa

    ReplyDelete
  9. Je mfano nikiamua kuacha nitaludishiwa nilichoweka (hisa yangu)

    ReplyDelete
  10. Akhsante sana kwa elimu nzuri๐Ÿ‘Š๐Ÿ‘Š

    ReplyDelete
  11. Asante Kuna elimu nimepata

    ReplyDelete
  12. Yaaan hisa sielew kabisa

    ReplyDelete
  13. Respect and I have a neat present: What Is House Renovation average cost to renovate a house

    ReplyDelete

Item Reviewed: Pata Elimu ya kutosha kuhusu "Hisa" na Namna ya Kumiliki hisa katika Kampuni. Rating: 5 Reviewed By: Unknown