Wachunguzi wa Uholanzi waliokuwa wanachunguza
chanzo cha ajali ya ndege ya Malaysia nchini Ukraine mwezi Julai
wanasema kuwa ndege hiyo ya abiria ilikumbwa na kitu chenye ncha na
kugongwa mara kadhaa na vifaa vyenye mionzi mikali.
Mwandishi wa BBC amesema kwamba ushahidi huo ni wa wazi na kwamba ndege hiyo ilishambuliwa kwa kombora.
Katika
ripoti yao ya kwanza ya kiuchunguzi ,maafisa hao wa Uholanzi
wanaojihussha na masuala ya usalama wa anga wameeleza kua hapakuwa na
tatizo la kiufundi lililosababisha ndege hiyo ipate ajali, ama makosa ya
rubani yalosababisha ndege hiyo kulipuka.
Wataalam hao wameendelea kueleza kwamba kisanduku cha kurekodia mwenendo wa ndege hiyo hakikuonesha kwamba kulikua na dharura.
Abiria
wote mia mbili na tisini na nane walipoteza uhai pindi ilipoanza safari
kutoka uwanja wa ndege wa Amsterdam kueleke Kuala Lumpur.Kutokana na
ajali hiyo kuna shaka kwamba vikundi vya waasi wa Urusi viliiidungua
ndege hiyo.
Lakini mpaka sasa Urusi imepinga kuhusika kwa namna yoyote na ajali hiyo.
Inaarifiwa kwamba ripoti kamili juu ya ndege hiyo MH17 itatolewa mwakani.
Chanzo:BBC.
KWA HABARI ZAIDI UNGANI NASI KWA KU-LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK.. Bonyeza hapa.
0 blogger-facebook:
Post a Comment