Msichana
wa miaka 18, raia wa India aliyetajwa kwa jina la Mangli Munda amefunga
ndoa na mbwa baada ya kulazimishwa na wazazi wake,
Wanaoamini kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kufukuza roho za kishetani na mikosi inayomsonga.
Inaelezwa
kuwa mbwa huyo alitafutwa na baba mzazi wa mrembo huyo na kufanyika
sherehe kubwa ikiwa na vitendo vyote vinavyofanywa na bibi harusi na
bwana harusi kwa taratibu zao za ndoa.
Kwa mujibu
wa Yahoo News, msichana huyo hakuwa na furaha kabisa na alieleza wazi
jinsi alivyochukizwa na kitendo hicho, “Siifurahii kabisa hii ndoa.”
Alisema binti huyo.
Bonyeza hiyo link hapo chini ;
“Tulilazimika
kutumia pesa nyingi kwa ajili ya hii ndoa. Hiyo ndiyo njia pekee
tunayoweza kufanya kuondoa mikosi aliyonayo na kufanya tendo jema kwa
ajili ya kijiji chetu.” Amekaririwa mama yake Munda.
0 blogger-facebook:
Post a Comment