JESHI
la Polisi nchini limetoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao vibaya
ikiwemo kutuma ujumbe wa matusi, uchochezi, picha za utupu sanjari na
kukashifu viongozi wa Serikali, dini na watu mashuhuri.Akizungumza
Dar es Salaam, Septemba 3,2014 Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema
kuwa tayari baadhi ya watu wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani
kujibu tuhuma hizo na wengine wanaendelea kuhojiwa.
“Kumejitokeza
tabia kwa baadhi ya watu kutumia mitandao ya kijamii na simu za
kiganjani kinyume na malengo yaliyokusudiwa kwa kusambaza taarifa za
uchochezi, kashfa,kuchafua viongozi wa Serikali.
“Wengine
wamekuwa wanasambaza picha utupu ambazo hazina maadili, hali ambayo ni
kosa la jina, ingawaje mwingine anaweza hasijue kuwa kufanya hivyo ni
kosa lakini sheria haitamuacha, alisema.
Senso
aliendelea kubainisha kuwa kuvunja kutofahamu sheria kwa kutoifahamu si
sehemu ya kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria, atakabainika kutenda
kosa hilo bila kujali anaifahamu sheria au la, atachukuliwa adhabu kali.
Alisema
oparesheni ya kuwabaini wanaosambaza ujumbe zinaendelea nchi nzima kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa lengo la
kuwakamata waharifu wa aina hiyo.
Aliongeza
kuwa hatua hiyo pia inawatia hatiani wale wote wanaotumia mitandao
kufanya utapeli na kujipatia kipato kwa watu mbalimbali nchini sanjari
na blogs zinazosambaza picha chafu ambazo ni kinyume na maadili.
“Wapo
baadhi ya watu wanatumia mitandao ya simu kutapeli watu na kujipatia
kipato, hivyo nao ni sehemu ya waharifu wanaotafutwa na jeshi la polisi
na yeyote atayekamatwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yake,” alisema.
Hivyo
alisisitiza kuwa Jeshi hilo linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na
uharifu huo, na kuwataka wale wanaotumiwa wa aina hiyo kutousambaza kwa
wengine bali waufute.
Pia
aliziomba kampuni za simu za mkononi pindi wanapoona ujumbe wa aina
hiyo wasiruhusu uende kwa mwingine ili nao wawe sehemu ya kupambana na
uovu huo.
0 blogger-facebook:
Post a Comment