728x90 AdSpace

­
Latest News
September 5, 2014

Bad News!! BINTI ABAKWA HADI KUFA BAADA YA KUDAI KUWA MIZENGO PINDA HAWEZI KUWA RAIS TANZANIA

Photo: Naona Trending Issue ni binti anayetajwa kwa jina la Bettie Ndejembi. Ambaye ninasoma huku na kule kuwa amefariki na kifo chake kikihusishwa na lugha za kuchafuana mitandaoni. Najaribu kuunga unga ninayosoma ila wala sipati kitu kamili........all in all, pole sana kwa familia ya mzee Ndejembi

Bettie Ndejembi enzi za uhai wake
Marehemu aliokotwa kwenye mtaro akiwa amefanyiwa vitendo vya kikatili na akiwa hajitambui


Wengi wadai mitandao ya kijamii (hasa Facebook, Twitter na Instagram) inatumiwa visivyo na walio wengi



Na Malisa Godlisten



Ninaandika makala haya nikitambua bayana kuwa yatamuudhi kila mtu anayeingia mtandaoni kwa minajili ya kuwanyanyasa wengine. Lakini siku zote ninaamini katika busara hii: kuuchukia ukweli hakubadilishi ukweli kuwa uongo. Ukweli ni ukweli na uongo ni uongo. Ukweli hauwezi kuwa uongo, na kadhalika uongo hauwezi kuwa ukweli. Kamwe asilani.



Wakati tunaomboleza kifo cha ndugu yetu Betty Ndejembi watu wamesema mengi, na yameandikwa mengi. Kila mmoja kwa namna alivyoguswa. Zitto Kabwe ametweet hivi asubuhi "Justice for Betty", akitoa rai haki ipatikane kwenye kifo cha Betty.


Jokate Mwegelo nae ametweet kuomba msaada wa kuchunguza kifo cha Betty. Na watu wengine maarufu kila mmoja kasema neno, labda kwa sababu Betty alikuwa maarufu in one way or another.


Lakini hatuwezi kukwepa ukweli kwamba siku chache kabla ya kifo chake, alinyanyaswa mno kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Japo hadi muda huu hatuwezi kuhusisha moja kwa moja uhusiano kati ya unyanyasaji huo na kifo chake, lakini mtu akinyanyaswa saa kadhaa kabla ya kifo chake, waweza kujenga picha flani.



Saa chache kabla ya kifo chake Betty alitweet kuwa "PINDA HAWEZI KUWA RAIS". Baada ya kutweet hakuonekana tena hadi alipookotwa mtaroni kesho yake asubuhi akiwa amefanyiwa vitendo vya kikatili na akiwa amepoteza fahamu.


Lakini kabla hata ya kutweet hivyo, Betty alikuwa anaandamwa sana mtandaoni huko Twitter. Kuna watu walianzisha team ya kumtukana, kumjibu hovyo na kumprovoke kwa kila alilofanya.


Naomba ieleweke kuwa simlaumu mtu kwa sababu sina mamlaka ya kufanya hivyo bali dhima ya makala haya ni rambirambi zangu kwa Betty kuzungumzia tatizo la unyanyasaji mtandaoni, sanjari na suala zima la unafiki kila kinapojiri kifo hususani cha mtu maarufu.

Tuna tatizo kubwa huko mitandaoni. Tumefika hatua ya kuwapa umaarufu watu wenye matusi ya nguoni, wazushi, wambeya, wanafiki. Wanaochafua wenzao, kutishia wenzao kwa kujifanya askari JKT,JWTZ au hata Polisi kusengenya na kupost majungu.... Aina ya binaadamu wanaostahili laana lakini twaishia kuwatukuza. 


Kwenye hii mitandao, matusi imekuwa njia ya mkato ya kupata umaarufu. Kuna wenzetu wengi tu wenye 'umaarufu' huko Twitter, Facebook na Instagram lakini ukidadisi chanzo cha 'umaarufu' huo, utaambiwa 'ah! huyu ana matusi si mchezo!'


Kuna watu wazima na akili zao wanatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii aidha kunyanyasa wenzao kama si kusherehesha unyanyasaji huo.



Marehemu Betty ni victim wa yote hayo. Alitukanwa sana, na aliitwa majina kadhaa ya kumdhihaki kabla ya kukutana na mauti. Kuna waliomwita Di Maria, superstar uchwara n.k.. na ninaamini hao waliomuita hivyo wanajifahamu na wengine wananisoma hapa.


Japo sijui chanzo cha 'ugomvi' wao, lakini naamini kuna watu wengi tu waliokuwa katika nafasi ya kuzima moto huo kwa vile walikuwa wakizifahamu pande zote mbili za 'ugomvi' husika lakini kwa sababu ya unafiki wakapalilia moto maana wanafurahi watu wakigombana.


La kukera zaidi ambalo ni wazi litajichomoza wakati wa maombolezo haya ni UNAFIKI. Watu walewale waliodiriki kumwandama marehemu wakati wa uhai wake watageuka kuwa wenye uchungu mkubwa baada ya kifo chake.



Hii inanikumbusha suala ambalo nimeshawahi kulizungumzia mara kadhaa kwamba 'wakati muafaka wa kutafuta vipaji vya uigizaji ni kwenye misiba: watu walewale waliokuwa wakikuchukia kwa nguvu zote watageuka wenye uchungu mkubwa kwa kifo chako.'

Ukiangalia baadhi ya tweets za mwisho za marehemu ni wazi kuwa binti huyo alikuwa anahitaji msaada kutoka kwa wanaomjali.


Mojawapo ya Tweet za mwishomwisho za marehemu alisema hivi "Do I have a sister to support me? No. Do I have a Dad/Mom to run to or support me. No. Im hurting and wanna cry? Yes. BUT I know God is watching"



Haihitaji shahada ya Saikolojia kujua kuwa Betty alikuwa kwenye kipindi kigumu mno na alihitaji msaada kwa watu waliokuwa karibu yake.



Betty anauliza"Nina dada wa kunisaidia? Hapana. Nina baba au mama wa kumkimbilia? Hapana. Nimeumizwa/nina uchungu na ninahitaji kulia (lakini nitamlilia nani?). Ila najua Mungu anaona"


 Isivyo bahati Betty hakuwa na baba, hakuwa na mama, hakuwa na dada wala kaka. Wote walishatangulia mbele ya haki. Alibaki peke yake, peke yake na Mungu wake.

Lakini binadamu wasivyo na aibu wala huruma wakazidi kumtukana na kumsimanga, huku wengine wakiporomosha matusi mazito. Hawakujua yaliyokuwa moyoni mwake. Wakamtambia kwa maisha mazuri wanayoishi na namna walivyobarikiwa.


Betty akiwa katika maumivu makali ya hisia akaposti hivi "Thank you all for the names i was called, lucky 'all have such a perfect life.! No hard feelings.. Im alive still.! Endeleeni kuongea"


Kwa tafsiri isiyo rasmi Betty alisema "Asanteni kwa majina yote mliyoniita. Mmebarikiwa kuwa na maisha mazuri.! Hamuumizwi na hisia kama mimi. Ila bado ninaishi, endeleeni kuongea"

 Isivyo bahati hakuna aliyejali, hadi juzi asubuhi (jumatano) Betty alipookotwa kwenye mtaro akiwa amefanyiwa unyanyasaji wa kijinsia na akiwa amepoteza fahamu.


Kifo cha Betty ni miongoni mwa vifo vya kikatili sana kuwahi kutokea nchini. Nashauri wanaharakati wa haki za wanawake wapambane kuhakikisha haki inapatikana. Akina Annanilea Nkya, Hellen Kijobisimba watafute haki ya binti huyu kama Zitto Kabwe alivyosema "Justice for Betty"


Fikiria mtu aliyekuwa kwenye maumivu makali ya hisia, anatekwa na genge la wahuni. Bila kujali kipindi kigumu alichokuwa anapitia, bila kujali hakuwa na wazazi, bila kujali 'psychological toacher' aliyokuwa nayo 'still' wakamfanyia unyanyasaji wa kijinsia hadi akapoteza fahamu.


Betty aliokotwa mtaroni na kupelekwa hospitali. Jana (alhamisi) aliweza kufungua macho, lakini hakuweza kuongea lolote hadi saa 3 usiku wa kuamkia leo, mauti ilipomkuta.


Kwaheri Betty, kwaheri classmate wangu (Majengo sec), kwaheri rafiki, kwaheri ndugu. Umeondoka dunia bado inakuhitaji. Naumia u have gone too young, lakini naumia zaidi coz umekufa kikatili mmno. Japo sijui nitakufaje, lakini nadiriki kusema hukustahili kifo cha aina hii.


Nakumbuka sms yako ya mwisho kwangu uliniambia hivi "Malisa blv me, only youths can change this country". Leo nilipopata taarifa ya kifo chako nimerudia kuisoma sms yako mara mbilimbili. Sikujua kuwa sms hiyo ndio ulikuwa unaniaga.



Umeniaga kwa kutuachia vijana wosia, kuwa vijana pekee ndio wenye uwezo wa kuibadilisha nchi hii. Nitakuwa nimekusaliti ikiwa sitautendea kazi wosia huu. I promise to fight and motivate other youths to liberate this country for ur dedication.



Umekwenda kumfuata mama yako, umemfuata baba yako. Wazazi wako walitangulia, leo wewe umewafuata. Hatimaye familia nzima mmekutana Paradiso.. 




Pumzika kwa amani Betty.!

ZAIDI KUHUSU MAREHEMU KWA MUJIBU WA  na Malisa Godlisten



Kuhusu alipookotwa Betty ni Mikocheni. Kuhusu utaratibu wa kuagwa ni kesho Muhimbili, kuhusu maziko yatafanyika Dodoma. Kuhusu waliokua wanamharass kwny social media ni pamoja na Diva wa Clouds fm (nimeattach post ya Diva inayoonesha as if kafurahia kifo cha Betty). 


Kuhusu umaarufu alikua mwanamitindo wa Swahili fashion together with Mustapha Hassanali na Jokate Mwegelo. Na ofcoz alishaanza kuwa maarufu kwny hayo mambo ya mitindo.
Anyway kama mnataka kujua umaarufu wake alikua mwanamitindo wa Swahili Fashion na partners wake wakiwa Mustapha Hassanali and Jokate Mwegelo. 
Waliouliza may be sio wafuatiliaji wa masuala ya fashion ndo maana hawamjui, but wengi wanaofuatilia issues za mitindo they know her.
Hatahivyo sijaandika makala hii kwa ajili ya umaarufu wake. Nimeandika coz nimeguswa sana na kifo chake. She was my schoolmate at Majengo, and last year she graduated UDOM, B.A International Relations bt akaamua kujikita kwny mambo ya modeling.
However sidhani kama ni sahihi kujua mtu ni nani ndo umtetee. Wote mliouliza huyu dada ana umaarufu gani, did u mean ktk kutetea haki inatakiwa kwanza umjue mtu? Km ndivyo mlivyomaanisha i think mmekosea. Either mnamjua Betty au hamumjui itz not an issue. The issue ni aliyofanyiwa. Je alistahili?
Tusiposema sisi tulio hai kwa kuwa tu hatumjui, nani atasema? Je mnataka Betty aibuke kutoka kwny mauti aje kutetea haki yake? Kumbukeni the dead cannot cry out for justice. It is a duty of the living to do so for them.!
So hata kama Betty angekua a mere citizen ktk nchi hii asiyejulikana na yeyote we could still plee for her justice. We could still shout "JUSTICE FOR BETTY
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: Bad News!! BINTI ABAKWA HADI KUFA BAADA YA KUDAI KUWA MIZENGO PINDA HAWEZI KUWA RAIS TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown