MAMBO
yanazidi kunoga katika dakika za lala salama kabla dirisha la usajili
halijafungwa – Arsenal wanakamilisha usajili wa Danny Welbeck kutoka
Manchester United kwa pauni milioni 16.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa England ameafikiana na Arsenal kuhusu maslahi yake
binafsi na atasaini mkataba wa miaka mitano kukipiga Emirates.
Klabu
hizo mbili pinzani zimefikia makubaliano ya kufanya biashara ya nyota
huyo mwenye umri wa miaka 23 na kuzima njozi za Tottenham ambayo nayo
ilikuwa ikisaka saini ya mkali huyo.
Welbeck atatangazwa rasmi kama mchezaji wa Arsenal muda mfupi ujao mara baada ya kufuzu vipimo vya afya.
0 blogger-facebook:
Post a Comment