Nchini Sierra Leone raia wameonekana kutekeleza agizo lililo wataka kukaa majumbani mwao kwa siku tatu mfululizo ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa ebola.
Mitaa na barabara nyingi zinazo kuwa na pilikapilika zimeonekana nyeupe ikiwa ni siku ya pili tangu utekelezaji wa agizo hilo uanze.
Ebola imekuwa tishio kwa mataifa ya Afrika magharibi ambapo mpaka sasa zaidi ya watu 2,400 wamesha poteza maisha kutokana na ugonjwa huo. Umoja wa mataifa umekuwa ukichukua hatua kuhakikisha inasaidia vita dhidi ya ebola huku Marekani hivi karibuni imetangaza mpango wake kabambe wakuhakikisha inatokomeza ebola Liberia.
Chanzo: BBC
0 blogger-facebook:
Post a Comment