Mwanamke
anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 amekufa papo hapo baada ya
kudondoka kwenye pikipiki aliyokuwa amepanda na kisha kukanyagwa na
gari.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura amesema kuwa ajali hiyo
ilitokea jana mchana katika barabara ya Bagamoyo eneo la Tangibovu
ambapo gari likiendeshwa na dereva asiyefahamika akitoka kwa Alysykes
kuingia barabara ya Bagamoyo, aliigonga pikipiki namba T 505 CTJ Fekon
ikiendeshwa na dereva asiyefahamika.
Alisema
pikipiki hiyo iliyokuwa ikitokea Mbezi Makonde kwenda Mwenge ilikuwa
imempakia mwanamke huyo ambaye baada ya pikipiki kugongwa alianguka
chini na kisha kukanyagwa na lori namba T 277 CIL aina ya Tata likiwa na
trela namba T 339 CYB lililokuwa katika uelekeo mmoja na pikipiki.
Kamanda
alisema mwanamke huyo alikufa papo hapo na mwili wake umehifadhiwa
katika Hospitali ya Mwananyamala huku Polisi wakiendelea kuwasaka
madereva waliohusika katika ajali hiyo.
KWA HABARI ZAIDI UNGANI NASI KWA KU-LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK.. Bonyeza hapa.
0 blogger-facebook:
Post a Comment