Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
VIONGOZI Wakuu wa Vyama vya siasa vyenye Wabunge vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) wamekuwa
katika mashauriano ya zaidi ya mwezi mmoja tangu tarehe 2 Agosti mwaka
huu huku wakishauriana juu ya mwenendo wa mchakato wa Katiba Mpya na
jinsi ya kuwa na uchaguzi ulio huru na wa haki hapo mwakaniAkiongea
kwa niaba ya viongozi wengine wa kituo hicho, Mwenyekiti wa TCD, Mhe.
John Cheyo amesema kuwa Katika mashauriano hayo yaliyochukua sura ya
Kamati ya Makatibu Wakuu, Kamati ya Wenyeviti wa Vyama vya CCM, CHADEMA,
CUF na NCCR-Mageuzi katika hatua tofauti.Mhe.
Cheyo ameeleza kuwa kamati zote zilitoa taarifa zao kwenye vikao vya
Viongozi Wakuu wa Vyama (Summit) ya TCD ambayo wajumbe wake ni
Wenyeviti, Makamu Wenyeviti na Makatibu Wakuu wa Vyama wanachama.
Mhe.
Cheyo aliongeza kuwa katika kutafuta maridhiano, Wenyeviti na Makatibu
Wakuu wa Vyama walifanya mashauriano na Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete siku ya tarehe 31 Agosti mwaka huu, hivyo tarehe Nane Septemba,
2014 hapa Dodoma wakatoa tamko lao.
“Pamoja
na kazi ya msingi inayofanywa na Bunge Maalum la Katiba, mchakato wa
Katiba unaoendelea sasa hauwezi kutupa Katiba itakayotumika katika
Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kuwa muda hautoshi kukamilisha mchakato na
kufanya mabadiliko yatakayohitajika ya Sheria, Kanuni na Taasisi
mbalimbali zitakazohitajika”, alisema Mhe. Cheyo.
Mhe.
Cheyo aliendelea kwa kusema kuwa, kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba mwisho wa mchakato ni kura ya maoni itakayofanyika mwezi Aprili
2015.
“Kama
itabidi kura irudiwe kwa mujibu wa Sheria iliyotajwa, kura itarudiwa
mwezi Juni au Julai 2015, muda ambao Bunge la Jamhuri ya Muungano
linatakiwa livunjwe kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2015 na ili
Katiba Mpya itumike katika uchaguzi Mkuu utakaokuja, itabidi uhai wa
Bunge na Serikali uongezwe zaidi ya 2015, jambo ambalo hatuliungi
mkono”, alisisitiza Mhe. Cheyo.
KWA HABARI ZAIDI UNGANI NASI KWA KU-LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK.. Bonyeza hapa.
0 blogger-facebook:
Post a Comment