Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo ambao ni Waandishi wa Habari mkoani
Mara Frolence Focus wa Mwananchi na Pendo Mwakembe wa Raia Tanzania
wamenusulika kwenye ajali hiyo wakiwa kwenye basi la Mwanza Coach
kutokea Musoma.
Mashuhuda
wamesema ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 5 asabuhi, baada ya basi
la Mwanza Coach lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza kugongana uso
kwa uso na basi la J4 lililokuwa likitoka Mwanza kwenda Sirari.
Zaidi
ya watu 45 wanasadikiwa kufariki dunia na wengine wengi wakijeruhiwa
vibaya baada ya mabasi mawili kugongana na kupinduka katika eneo la
Sabasaba nje kidogo ya mji wa Musoma, mkoani Mara.
Wamesema
mabasi hayo ambayo yote yalikuwa kwenye mwendo kasi yalikutana kwenye
daraja dogo katika eneo hilo huku pia gari dogo aina ya Land Crusser
likitaka kuovateki na hivyo kupelekea kutokea kwa ajali hiyo. Mmoja wa
mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa jina la Juma Nyamhanga amesema
alisikia kishindo kikubwa muda mfupi baada ya kutokea kwa ajali hiyo na
baadae kusikia vilio vikitokea ndani ya mabasi hayo.
Akizungumzia kwa tabu akiwa amelazwa kwenye wodi namba 4 hospitali ya
rufaa ya mkoa wa Mara, Frolence amesema walishangaa kuona abiria
waliokuwa wamekaa mbele wakisimama na kurudi nyuma na ghafla akasikia
mlio mkubwa.
Akizungumza nje ya chumba cha (ICU) kwa niaba ya
Mganga Mkuu, Dakatari Martini Khani amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo
na kudai kuwa wamepokea idadi kubwa ya maiti na majeruhi huku idadi
kamili ikiwa bado haijafahamika.
0 blogger-facebook:
Post a Comment