Kiingilio
cha chini kwenye mechi ya Ngao ya Jamii kuashiria uzinduzi wa msimu
mpya wa Ligi kati ya Azam na Yanga itakayochezwa Jumapili (Septemba 14
mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.
Mechi
hiyo itaanza saa 10 kamili jioni, na kiingilio hicho cha sh. 5,000 ni
kwa viti vya rangi ya kijani na bluu vitakavyochukua jumla ya watazamaji
36,000 katika uwanja huo wenye viti 57,558.
Viingilio
vingine katika mechi hiyo ambayo itatumia tiketi za elektroniki ni sh.
10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa viti vya VIP C na B
wakati viti vya VIP A kiingilio ni sh. 30,000.
MWAMUZI LUGENGE KUAGWA LEO
Mwamuzi
wa daraja la kwanza (class one), Luteni Godwill David Lugenge
aliyefariki dunia juzi (Septemba 7 mwaka huu) kwa ajali ya gari katika
Wilaya ya Handeni mkoani Tanga anaagwa leo (Septemba 9 mwaka huu).
Mwili
wa marehemu ambao umehifadhiwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH)
Lugalo, baadaye leo saa 6 mchana utapelekwa nyumbani kwa kaka yake
Kimara Bucha jijini Dar es Salaam ambapo shughuli za kuaga zitafanyika
kabla ya safari ya kwenda mkoani Njombe kwa ajili ya mazishi.
Luteni
Lugenge ambaye mwishoni mwa wiki alishiriki mitihani ya utimamu wa
mwili kwa waamuzi wa Ligi Kuu, akiwa na ndugu yake Christopher Alexander
Lunyungu katika gari dogo walipata ajali hiyo wakati wakienda mkoani
Kilimanjaro.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambalo limetoa ubani wa sh. 200,000
kwa familia ya marehemu kwenye shughuli ya kuaga itawakilishwa na mjumbe
wake wa Kamati ya Utendaji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Waamuzi, Saloum Umande Chama.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Luteni Lugenge, Chama cha Waamuzi
wa Mpira wa Miguu nchini (FRAT) na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha
msiba huo mzito. Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.
KWA HABARI ZAIDI UNGANI NASI KWA KU-LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK.. Bonyeza hapa.
0 blogger-facebook:
Post a Comment