USAJILI: Chicharito Ajiunga na Real Madrid kwa Mkopo.
Akiwa na jezi yake mpya ya Real Madrid na Rais wa klabu hiyo Perez
Wakati akichukuliwa vipimo vya afya na kubainika yupo fiti
Akiangunga saini ya kuichezea klabu hiyo bingwa ya Ulaya
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Mexico, Javier Harnendez Chicharito
amefaulu vipimo vya kujiunga na klabu ya Real Madrid na amekabidhiwa
jezi namba 14 kwa ajili ya kuichezea wababe hao wa Ulaya kwa mkopo
akitokea klabu yake ya Manchester United.
Chichirito ambaye hakuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza cha
Mashetani Wekundu tangu alipotua akitokea kwao Mexico, amejiunga na
Madrid akimpisha Ramadel Falcao aliyetokea Monaco aliyetua Old Trafford
kwa mkopo vilevile.
Mshambuliaji huyo alitua Old Trafford mnamo mwaka 2010 na amenyakuliwa na
Madrid ili kuchukua nafasi ya Alvaro Morata ambaye aliuzwa Juventus.
0 blogger-facebook:
Post a Comment