Wengi wetu tumekuwa tukiandikiwa kipimo cha X ray kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa na matatizo mbalimbali na tumekuwa tukifanya mara kwa mara bila kujua madhara yake hivyo tunashauriwa kupiga picha hizi za x ray pale penye umuhimu tu na kwa maelekezo ya madaktari ili kuepuka madhara yatokanayo na teknologia hii ya mionzi mikali kama ifuatavyo:
1. Watoto wadogo wanapopigwa picha za X ray chini ya tumbo bila kuvaa nguo za kuwakinga na mionzi hii kuna uwezekano mkubwa wa kuharibu mfumo wao wa uzazi na hivyo kusababisha utasa maishani..
2. Mama mjamzito anapopigwa X ray tumboni kuna uwezekano wa kumuhathiri mtoto aliye tumboni asa kupata saratani ya damu, tezi, na magonjwa ya moyo na kisukari..
3. Kupiga X ray mara kwa mara uharibu na kusababisha kansa ya mifupa na ngozi
Kumbuka unapaswa kuongea na daktari wako mapema ili kuona kama kuna uwezekano wa kufanya vipimo vingine badala ya X ray au kuvaa vifaa vya kukukinga na mionzi kwa ajili ya kuepuka madhara haya.
.
USIPITWE NA MENGI KUHUSU AFYA YAKO UNGANA NASI KWA KU-LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK.. Bonyeza hapa.
0 blogger-facebook:
Post a Comment