Taarifa
za kutisha zimeibuka kutoka mjini Bama moja ya miji ambayo ilitekwa na
wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram Kaskazini Mashariki ya Nigeria
Seneta mmoja wa eneo hilo,Ahmed Zanna, aliambia BBC kwamba wakazi hawaruhusiwi kuwazika jamaa wao waliouawa na wapiganaji hao.
Inaarifiwa miili imetapakaa katika barabara za mji huo ambao Boko Haram imeuteka.
Kundi hilo linasemekana kuuteka mji huo huku wapiganaji wa kundi hilo wakishika doria katika barabara zake.
Maelfu ya watu wametoroka huku idadi kubwa ya wengine wakiuawa.
Seneta
huyo ameitaka serikali ya Nigeria kupeleka wanajeshi mjini Maiduguri
ambao ni mji mkuu wa jimbo hilo ili kuulinda dhidi ya wapiganaji hao.
Mnamo siku ya Jumatano serikali ya jimbo hilo ilikanusha madai kuwa jimbo hilo limetekwa na wapiganaji hao.
Maafisa wakuu wanakisia kuwa watu 26,000 wameachwa bila makao kutfuatia mapigano katika mji wa Bama.
Bwana
Zanna anasema kuwa barabara za mji huo zimejaa miili ya watu na Boko
Harama imewakata wakazi kuwazika jamaa wao. ''Kwa hivyo hali ni mbaya na
inaendelea kuzorota,'' asema bwana zANNA
Boko
Haram wameteka miji kadhaa Kaskazini Mashariki ya Nigeria, katika miezi
ya hivi karibuni na kusababisha hofu kuwa huenda wakaufikia mji mkuu
Maiduguri.
Bwana
Zanna amesema kuwa itakuwa janga kubwa ikiwa Boko Haram wataushambulia
mji wa Maidiguri ambao una watu zaidi ya milioni mbili.
0 blogger-facebook:
Post a Comment