728x90 AdSpace

­
Latest News
September 6, 2014

Baraza la Ma-Askofu Katoliki Kenya latoa Tamko Juu ya Hari ya Taifa la Kenya


Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Kenya(KCCB),kupitia Tume yake ya Haki na Amani, lilitoa tamko lake lenye jina, "Uwajibikaji wa Viongozi katika Umoja na Usalama wa Nchi Yetu”mbele ya mkutano wa vyombo vya habari, katika mtazamo wa kutoa mwanga katika kile kinachoendelea ndani ya marubano ya kisiasa nchini Kenya. 

Maaskofu walitoa tamko lao kwa wana habari baada ya majadiliano yao katika mkutano wao wa mwaka uliofanyika Kwale katika Jimbo Kuu la Mombasa. Tamko hilo, limeangalishwa katika Injili ya Luka12:28 “Na kila aliyepewa vingi kwake, huyo vitatakiwa vingi, naye walimwekea amana vitu vingi , kwake huyo watataka na zaidi".

Tamko la Maaskofu limeanza na salaam za rambirambi za dhati kwa familia za wahanga na watu wa Kata ya Mandera, ambako kulifanyika mauaji ya hivi karibuni na migogoro baina ya koo ambavyo vinamesababisha uharibifu mkubwa wa maisha na mali. 


Na kwamba , kama Tume ya Amani, wana wasiwasi na kujali uwepo wa mfumo au utaratibu wa kutoa silaha za moto kwa makundi mbalimbali wanamgambo, na hasa uhamasishashi wa ubabe kwa makundi ya vijana, migogoro na mauaji mengi, yanayofanyika katika makazi ya watu na uharibifu wa mali , kama inavyo shuhudiwa katika Wilaya mbalimbali. 

Maaskofu wanasema uhalifu huu wa kutisha halikubaliki kabisa. Kila maisha mtu yana thamani isiyoweza kuwa na mbadala. Nahivyo wamezitaka pande zote kuacha utamaduni huu wa kifo. Na kwamba chuki na fitina za kutaka kulipiza kisasi, "Jicho kwa jicho” ni kuleta tu upofu wa kuendeleza vurugu.

Hivyo Maaskofu wanasema, wakati umefika kwa Wakenya kuona umuihimu wa kuachana na matendo yasiyokuwa na maendeleo, badala yake wajihusishe zaidi katika utendaji kwa maslahi ya taifa na si kwa maslahi ya mtu binafsi au makundi ya kisiasa . Viongozi wote wanatakiwa kuhamasisha utendaji wa mazuri kwa manufaa ya watu wote wa Kenya.

Wakenya kwa masikitiko walishuhudia mapambano makubwa ya wanasiasa wakati wa uchaguzi katiak ngazi zote , tangu madiwani, wabunge, Maseneta, Wanawake Wawakilishi, Magavana na viongozi wa kitaifa kwa gharama watu wa Kenya. 


Na kwamba Tume Katoliki ya haki na amani, ina ufahamu wa mizizi ya kihistoria katika masuala ya ardhi Kenya. Jambo hili imebakia kitendawili kwa kila jaribio la serikali inayopita huliacha bila kupta suluhu.
 

Kwa hiyo, Tamko la Maaskofu limetoa mapendekezo yake kama ilivyoshauriwa na Tume Katoliki ya haki na amani katiak yafuatayo kwamba tabaka la wanasiasa, ni lazima kujenga mashauriano na uelewa juu ya suala la kura ya maoni ili kuhakikisha kwamba ni kwa ajili ya maslahi ya Wakenya na si kutumikia maslahi yao wenyewe.

Na juu ya suala la ardhi, serikali na taasisi zake lazima kutekeleza mfumo wa kina kama ilivyo elekezwa katika Katiba ya Kenya, 2010 na sheria ya baadae juu ya nchi, na hivyo Serikali inapaswa kutekeleza mapendekezo ya Ripoti ya Ndung'u na ripoti ya Tume ya Ukweli, Haki na Maridhiano.

Tamko linawakumbusha Wakenya wote kwamba, ulinzi na usalama ni wajibu wa kila mtu. Suala la usalama halina mzaha. Viongozi wote wa chama tawala cha muungano na upinzani ni lazima kuungana na kutenda kwa pamoja ili nchi idumu katika hali ya usalama na amani. Kwa maana hiyo kila kiongozi aliyechaguliwa na wananchi ni lazima atimize wajibu wake kwa mujibu wa Katiba katika kuwatumikia Wakenya na kuondokana na ushindani wa kung’ang’ania madaraka katika uwanja wa kisiasa.

Pia tamko la Maaskofu limeonyesh akujali ukosefu wa ajira kwa vijana, kwamba inaendelea kubaki tishio kwa usalama! Kwa hiyo ni lazima jitihda zaidi zifanyike kupata ufumbuzi wa tatizo hili iwe kimafunzo au katiak juhudi za maendeleo. Na utawala ni uwe mstari wa mbele katiak kuhakikisha ushiriki wa wananchi katika masuala ya maendeleo.

Na mwisho tamko linatoa wito kwa Wakenya wote, kuwa mlizi wa mmoja kwa mwingine, kw akuwa taifa la Kenya ni rasilimali yao wote , nahivyo ni lazima kutumia vyema na kuilinda.
Mungu ibariki Kenya.
 

Tamko limetiwa na Saini na: Askofu Mkuu wa Kisumu na Mwenyekiti wa Tume ya Haki na amani ya KCCB – Askofu Mkuu Zakayo Okoth; Askofu i Cornelius Korir, wa Jimbo la Eldoret ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti waTume Katoliki ya Haki na amani KCCB; Askofu wa Machakos na Mjumbe wa Tume, Askofu Martin Kivuva Musonde, pamoja na wawakilishi kutoka Chama kinachounganisha Mashirika Katoliki ya Masista Kenya (AOSK) na mwakilishi kutoka mwavuli unaouganisha Wakuu wa Mashirika ya Kidini Kenya (RCSK).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: Baraza la Ma-Askofu Katoliki Kenya latoa Tamko Juu ya Hari ya Taifa la Kenya Rating: 5 Reviewed By: Unknown