Mara
baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara, Mshindi wa Shindano la
Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago akitoa Maneno ya
Shukrani kwa Wakazi wa Mtwara waliojitokeza kuja Kumpokea uwanja wa
Ndege wa Mtwara mapema Leo. Vilevile alitoa Shukrani zake zote kwa
Watanzania Wote kwa Kuweza umpigia Kura na Kumfanya aibuke mshindi wa
Milioni 50 za Tanzania katika fainali ya Shindano la Kusaka vipaji vya
Kuigiza lijulikanalo Kama Tanzania Movie Talents (TMT).
Wapenzi,
Mashabiki na wana Mtwara wakiwa Nje ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara
wakisubiri Kumpokea Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT)
2014 Mwanaafa Mwinzago kwaajili ya Kumpongeza kwa Kuibuka MShindi wa
SHilingi Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Shindano la Tanzania
Movie Talents (TMT)lililofanyika Mwisho wa Mwezi wa nane katika Ukumbi
wa Mlimani City, Jijini Dar Es Salaam.
Wakazi
wa Mkoa wa Mtwara wakimpongeza Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago
ambaye amewasili Mkoani Mtwara ambapo ndio Nyumbani Kwao akitokea Dar Es
Salaam mara baada ya Kuibuka Mshindi na Kujinyakulia Kitita Cha
Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
Ndugu,
Jamaa na Marafiki wa Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakipiga
picha ya Pamoja mara baada ya Kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara
akitokea Dar Es Salaam.
Shangwe
na Ndelemo zilitawala katika Viunga Vya Uwanja wa Ndege wa Mtwara kabla
na Baada ya Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014,
Mwanaafa Mwinzago kutua katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara akitokea Dar Es
Salaam ambapo fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT)
lilifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City.
Msafara wa Kuelekea Nyumbani Kwa MShindi wa TMT 2014 , Mwanaafa Mwinzago Ukitoka katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
Msafara Ukielekea Nyumbani kwa Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago,
Wazee
kwa Vijana wakimpongeza Mwanaafa Mwinzago wakati alipokuwa akipelekwa
Nyumbani Kwao kwa Msafara wakati akitokea Uwanja wa Ndege
Wakazi
wa Mtwara wakimpongeza Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakati
alipokuwa akipita na masafara uliompokea uwanja wa Ndege wa Mtwara na
kumsindikiza Hadi Nyumbani kwao Magomeni Mkoani Mtwara mapema leo
Asubuhi
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi wakimpongeza Mwanaafa Mwinzago wakati alipokuwa
akipita na msafara kutoka Uwanja wa Ndege wa Mtwara akielekea Nyumbani
kwaajili ya Kujiandaa kwenda Shule leo asubuhi wakati alipowasili
kutokea Mkoani Dar Es Salaam.
Majirani,
Ndugu, Marafiki na Wakazi wa Mtwara wakimshangilia Mshindi wa TMT 2014
Mwanaafa Mwinzago wakati alipowasili Nyumbani Kwao Eneo la Magomeni ,
Manispaa ya Mtwara Mikindani akitokea Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
KWA HABARI ZAIDI UNGANI NASI KWA KU-LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK.. Bonyeza hapa.
0 blogger-facebook:
Post a Comment