728x90 AdSpace

­
Latest News
September 6, 2014

DR. MWAKYEMBE AAMURU MABASI YALIYOSABABISHA AJALI MKOANI MARA YAFUNGIWE MARA MOJA.

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe ameagiza makampuni ya Mabasi ya J4 Express na Mwanza Coach yafungiwe mara moja..
 

Dk Mwakayembe amesema sehemu iliyotokea ajali na kusababisha vifo vya watu 39 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa ni sehemu ambayo kila dereva alikuwa akimuona mwenzake, hivyo ulikuwa ni uzembe wa hali ya juu.
 

“Ile sehemu ipo wazi kabisa, kule kuna kilima na huku kuna kilima na daraja lipo katikati, kwa hiyo wale madereva walikuwa ni wazembe na uzembe kama huu unasikitisha sana.

Walikuwa wanaonana na hata lile gari dogo walikuwa wanaliona… hii hali inasikitisha sana,” alisema Dk. Mkwakyembe.  


Alitahadharisa kwamba kuanzia sasa hivi kila basi litakalopata ajali ya kizembe ataaamuru vyombo husika vilifungie ili kuokoa maisha ya wananchi.
 

“Katika uongozi wangu madereva wazembe wajuwe kabisa kuwa sitaweza kuvumilia, nitaamuru wafungiwe mara moja wakisababisha ajali za kizembe,” alisisitiza Waziri Mwayembe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: DR. MWAKYEMBE AAMURU MABASI YALIYOSABABISHA AJALI MKOANI MARA YAFUNGIWE MARA MOJA. Rating: 5 Reviewed By: Unknown